TTCL

Habari

​LATEST UPDATE: Majeruhi wetu 3 wanaendelea vizuri  nchini Marekani. 

on

MTOTO Wilson, anayeonekana hapo chini  kwenye picha ya kwanza, leo ameanzishiwa mazoezi ya viungo 
(Therapy), baada ya zoezi la UPASUAJI kukamilika, na MADAKTARI wamesema leo kwa mara ya KWANZA ameweza KUKAA mwenyewe kwenye kitanda chake, na kwamba alikuwa amejawa na TABASAMU kubwa***

MTOTO Sadia (anayeonekana kwenye picha ya pili ameanzishiwa mazoezi ya VIUNGO (Therapy) leo baada ya zoezi la UPASUAJI kukamilika. MADAKTARI wamesema MTOTO Sadia leo kwa mara ya KWANZA ameweza KUSIMAMA mwenyewe, na waliona kama MUUJIZA, na ameweza KUONGEA vizuri***

MTOTO Doreen (picha haijawekwa), amepewa MAPUMZIKO maalumu Siku Nzima ya leo akiwa anaandaliwa tayari kwa UPASUAJI wa uti wa mgongo ‘spine’ kesho, ALHAMISI mapema ASUBUHI*** 

Tuendelee KUWAOMBEA. (Picha kwa hisani ya D. Meyer, Sioux City IA).

UJUMBE KWA FACEBOOK