Habari

MTENDA AWANUFAISHA WAKULIMA WA MPUNGA

on

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene akikagua mchele unaouzwa na Kampuni ya Mtenda alipotembelea banda la maonesho ya nanenane hivi karibuni. Waziri George Simbachawene akimpongeza mkurugenzi wa Mtenda rice company George Mtenda baada ya kutembelea banda lake katika maonesho ya nanenane yaliyomalizika hivi karibuni jijini Mbeya George Mtenda akiwa katika Banda la kuuzia mchele katika maonesho ya Wakulima nanenane jijini Mbeya Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mtenda wakiwa tayari kuwahudumia wateja wa mchele Mchele unaochakatwa na kuongezewa thamani na Mtenda tayari kwa kuuzwa katika masoko ya nje na ndani kama unavyoonekana.

ZAIDI ya Wakulima 10500 wa zao la Mpunga mkoani Mbeya wamenufaika na mafunzo ya kilimo bora na chenye tija ikiwa ni katika kufanikisha malengo ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa Mtenda Rice company, George Mtenda alisema baada ya kuona wakulima wakipanda mazao yao pasipokuzingatia kanuni za kilimo bora akaona ni vema akatoa elimu kabla ya kununua mazao yao.

Alisema mpango huo alianza kuutoa kwa wakulima mwaka 2008 ambapo aliweza kuwafikia wakulima hao katika Wilaya za Kyela, Mbarali na Momba ambao hivi sasa wanauza mpunga ambao huongezewa thamani na Kampuni ya Mtenda na kufungashwa katika ubora wa hali ya juu.

Alisema baada ya kununua mpunga kutoka kwa wakulima hao ambao wamefundishwa na kuwezeshwa kupitia wadau mbalimbali na kuwa na uhakika wa soko kutokana na kununua yeye mwenyewe kisha kuukoboa na kuupanga kwenye madaraja mbalimbali tayari kwa kuuzwa ndani na nje ya nchi.

Baadhi ya wakulima walionufaika na elimu hiyo walimpongeza Mtenda kwa kuwaona na kuongeza kuwa baada ya elimu hiyo wameona manufaa mazuri kwani hulima kwa tija kwa kufuata kanuni bora za kilimo.

Mwisho.

UJUMBE KWA FACEBOOK