TTCL

Makala

JE WAJUA……….. KUNA KITU KINAITWA ”CHAI YA MAJANI YA MPAPAI’   

on

       Majani ya mpapai ni mazuri katika kuongeza ufanisi wa insulini. Ni mazuri kwa watu wenye kisukari cha aina ya pili. Pia majani ya mpapai husaidia kupunguza matatizo yawezayo kuwatokea watu wenye kisukari, matatizo kama vile mafuta kwenye ini, matatizo katika kibofu cha mkojo na pia husaidia kupunguza mfadhaiko/stress. Kuna faida nyingine kubwa zaidi ya kutumia majani ya mpapai ambayo ni uwezo wake katika kutibu vidonda vitokanavyo na kisukari kwa haraka zaidi. Waganga wengi wa tiba asili kutoka Japani na Australia Na wengine wengi toka mataifa mbalimbali wamekuwa wakitumia majani ya mpapai kutibu kisukari kwa miaka mingi sasa.

Mahitaji:

• Majani 10 ya mpapai

• Maji lita 2 

Maandalizi:

• Tumbukiza hayo majani ya mpapai katika maji.

• Chemsha hayo majani katika maji kwenye moto hadi maji yatakapobaki nusu yake (lita 1).

• Ipuwa na uache ipowe

• Kunywa maji haya kidogo kidogo kutwa nzima. Fanya hivi kwa mwezi mmoja mpaka miwili.

Juisi hii ya majani ya mpapai iliyoandaliwa kwa mtindo huu ni nzuri katika kuondoa sumu mwilini na kurekebisha afya yako kwa ujumla huku ikirekebisha matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kuongeza kinga ya mwili wako. Share na wengine wapate afya

UJUMBE KWA FACEBOOK