TTCL

Habari

ACT WAZALENDO WAONYA WATENDAJI WABAGUZI

on

Viongozi waandamizi wa Chama cha ACT Wazalendo wakiwa kwenye kikao cha kujadili mikakati ya kuwafikia wanachama waoKatibu mwenezi na Mawasiliano wa ACT Wazalendo Mkoa wa Songwe Michael Nyilawila (katikati) akiongoza kikao cha viongozi waandamizi wa chama hicho  Viongozi waandamizi wa ACT Wazalendo wakionesha ishara ya Chama chao baada ya kumaliza kikao kifupi kilichofanyika Mlowo mkoani Songwe

 

CHAMA cha ACT Wazalendo kimewataka viongozi wa Serikali za Vijiji Mkoa wa Songwe kushirikiana na viongozi wa vyama vya siasa katika shughuli za maendeleo bila ubaguzi.

 

Wito huo ulitolewa juzi na Katibu Mwenezi na mawasiliano wa Chama hicho Mkoa wa Songwe, Michael Nyilawila wakati wa kikao maalum cha viongozi waandamizi wa ACT Wazalendo mkaoni hapo.

 

Alisema Chama kinaunga mkono jitihada na juhudi za Rais Dk. John Magufuli katika utendaji wake ambao umelenga katika kuwaletea maendeleo wananchi wote bila kujali ubaguzi wa vyama vya siasa.

 

“Rais anasema maendeleo hayana vyama hivyo hata sisi tunakubaliana nae katika kuwatumikia wananchi isipokuwa viongozi wa huku chini kama Watendaji ni wabaguzi na wanatabia ya kufukuza raia kwenye maeneo yao waache” alisema Nyilawila.

 

Aliongeza kuwa Chama kimejipanga kutoa elimu kwa wananchi ili wajue Chama kinachoshughulikia maslahi ya wananchi ya moja kwa moja ni ACT Wazalendo tofauti na vyama vingine ambavyo viongozi wake wanafuata maslahi binafsi.

 

Hata hivyo alisema piaChama kimejipanga kusimamisha wagombea Udiwani wa Kata tano katika Mkoa wa Songwe endapo tume itatangaza uchaguzi wa marudio kufuatia waliokuwa madiwani kupitia Chadema kutimkia CCM.

 

Nae Katibu wa Vijana wa Chama hicho Mkoa wa Songwe, Nestory Tweneshe alisema Chama kinaendelea kuimarisha ngome ya vijana na kuwaandaa kuwa viongozi wa baadae.

 

Alisema hivi sasa hamasa ya vijana kujiunga na Chama ni kubwa hivyo Chama kinakuwa karibu nao kuhakikisha hawavunjiki moyo wa kurudishwa nyuma na vitendo vinavyoendelea vya viongozi kuhamahama.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Mbozi, Viniwa Mahenge alisema endapo Makao makuu ya Chama hicho yataruhusu kushiriki uchaguzi mdogo tayari kama Chama kinao vijana wanaoweza kusimama na kushinda uchaguzi huo.

 

Baadhi ya Kata ambazo ziko wazi baada ya madiwani wake kutimkia CCM kutoka Chadema ni pamoja na Kata ya Mpona iliyopo Wilaya ya Songwe, Mpemba Wilaya ya Momba, Kaloleni, Sogea, Majengo na Mwaka Kati zote katika mji mdogo wa Tunduma.

 

Mwisho.

UJUMBE KWA FACEBOOK