TTCL

Habari

BABA MKUBWA AMJERUHI MTOTO WA MDOGO WAKE

By

on

Baba mkubwa aliyetajwa kwa jina la Mohamed Said a.k.a Muddy, mkazi wa Tegeta-Msufini jijini Dar amepigwa pingu akituhumiwa kumfanyia ukatili wa kutisha wa kumsulubu mtoto wa kiume wa mdogo wake, mwenye umri wa miaka 6( jina linahifadhiwa).  Inadaiwa kuwa Muddy alimchukua mtoto huyo kutoka kwa wazazi wake wanaoishi mkoani Mtwara kwa lengo la kuja naye Dar kwa ajili ya kumsomesha lakini kinyume na lengo hilo, jamaa huyo alipomfikisha Dar ilidaiwa alianza kumfanyia ukatili mtoto huyo wa dozi ya vipigo.  Majirani walisema kuwa jamaa huyo amekuwa akimshushia kipigo mtoto huyo mara kwa mara kwa kutumia bomba la plastiki na waya wa umeme huku adhabu kama kumnyanyua miguu juu kichwa chini, kumnyanyua juu kwa kumshika masikio na kushinda muda mrefu bila kula vikiwa ni sehemu ya maisha ya mtoto huyo.Una lipi la kusema juu ya tukio kama hili?

UJUMBE KWA FACEBOOK