TTCL

Habari

CBE MBEYA YAJIVUNIA MAFANIKIO.

on

CHUO cha Elimu ya Biashara(CBE) Kampasi ya Mbeya kimeupongeza mtandao wa Mbeya yetu kwa kufanikisha idadi kubwa ya wanafunzi kujiunga na Chuo hicho katika mwaka wa masomo 2016/2017.

Akizungumza na www.mbeyayetu.co.tz, Mhadhiri msaidizi wa CBE, Mr.Beny Benjamin alisema tangu waanze kutangaza nafasi za masomo katika mtandao huu mwitikio umekuwa mzuri tofauti na kutumia njia zingine.

Alisema katika mwaka wa masomo 2015/2016 mwitikio ulikuwa ni mdogo tofauti na mwaka wa masomo 2016/2017 ambapo idadi kubwa ya vijana walijitokeza katika kujiunga nafani mbalimbali.

Aidha alitoa wito kwa Wahitimu wa Kidato cha nne na kidato cha Sita kujitokeza kuomba nafasi za masomo kwani bado Chuo kinaendelea kupokea wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/18 katika fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, masoko na uendeshaji wa biashara (Certificate & Diploma) ambapo nafasi hizo zinaombwa moja kwa moja chuoni au kwenye mtandao wa chuo ambao ni  www.cbe.ac.tz

Alisema Chuo kinapatikana Forest ya Zamani kilipo Chuo kikuu kishiriki (Open University) au kwa maelezo zaidi kuhusiana na Chuo hicho wasiliana kwa namba 0744 – 762825.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK