TTCL

Habari

CCM MBEYA MJINI WAPATA UONGOZI MPYA

on

Katibu wa CCM, Mbeya mjini, Gerald Mwadalu akitoa maelekezo ya kanuni za Uchaguzi wa nafasi mbalimbali ndani ya Chama hicho ngazi ya Wilaya ya Mbeya mjini wakati wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Mbeya mjini, Ephraim Mwaitenda akiwaaga Wanachama wa Chama hicho kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya uliofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Mmoja wa  wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti Wilaya ya Mbeya mjin, Eden Katininda akiomba kura kwa wanachama waliofika kwenye uchaguzi.Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya mjini wakitambulishwa na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Ephraim Mwaitenda. Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa CCM wakifuatilia zoezi la uchaguzi la kuwapata viongozi wapya wa Wilaya ya Mbeya mjini.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Mbeya mjini imepata safu ya viongozi wapya wataongoza kwa miaka mitano kutokana na uchaguzi  uliofanyika na kumalizika mwishoni mwa wiki hii.

Uchaguzi huo ambao ulikuwa ukichagua viongozi kuanzia ngazi ya Mwenyekiti wa Wilaya, Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wilaya, Wajumbe watatu wa kuwakilisha Wilaya kwenye mkutano mkuu Taifa, Wajumbe wawili kuwakilisha mkutano mkuu wa Mkoa na Wajumbe 10 wanaounda Halmashauri kuu ya Wilaya na wajumbe watatu wa Kamati ya Siasa Wilaya.

Akitangaza viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyioka katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine na Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mbeya, Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya mjini, Gerald Mwadalu alisema nafasi ya Mwenyekiti ilinyakuliwa kwa kishindo na kijana wa miaka 28 Affrey Nsomba akiwabwaga wakongwe Akim Mwakalindile na Eden Katininda.

Alisema nafasi ya Katibu wa siasa Itikadi na Uenezi ilikuwa na washindani wanne ambapo Philimon Mng’ong’o alifanikiwa kutetea nafasi yake kwa kujinyakulia kura 82 dhidi ya Juma koko aliyepata kuira 27, Fulco Mlelwa aliyepata kura 9 na Joyas Ngajigwa ambae hakuambulia kitu.

Alisema nafasi ya mkutano mkuu Taifa kuwakiliosha Wil;aya ilichukuliwa na Charles Mwakipesile, Lucy Sitta na Suleiman Haroub na kuwabwaga Atupele Kakyela, Jacklson Numbi, Maulid Issah, Michael Mbuza, Nwaka Mwakisu na Richard Shanhvi.

Wadalu alisema wawakilishi wawili wa Mkutano mkuu wa Mkoa zilichukluliwa na Suzana Simkoko na Tumwitikege Sanga wakiwabwaga watu watano ambao ni Godfrey Kapunga,Habaya Sintufya, Jackson Numbi, Joyce Stambuli na Maria Nyagawa.

Aidha aliwataja waliofanikiwa kupita katika Halmashauri kuu ya wilaya ambao ni kumi kati ya 30 ambao majina yao yalipita kwenye mchujo  KUWA NI Abdalah Kilanga,Alen Mbuza, Charles Mwakipesile,Edith Kapwela, Fortunatus Tapule,Lyidia Gunda,Malanyingi Matukuta,Mary Mwaijumba,Shabani Chalo na Tumwitikege Sanga.

Akizungumza baada ya ushindi Mwenyekiti Affrey Nsomba aliwaomba wanachama wa CCM Wilaya ya Mbeya mjini kumpa ushirikiano katika uongozi wake ili waweze kufanikiwa kuligomboa Jimbo ambalo linashikiliwa na Joseph Mbilinyi (Chadema).

Hata hivyo wagombea wenza wa nafasi hiyoAkim Mwakalindile na Eden Katininda walisema uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na mshindi kukiuka kanuni za uchaguzi kwa kupiga kampeni za wazi na kutochukuliwa hatua zozote.

Walisema kutokana na hali hiyo tayari wamemwandikia barua Katibu wa CCM Wilaya na nakala kupeleka ngazi ya Mkoa na Taifa kwa hatua zaidi ikiwemo kufuta matokeo hayo na kurudiwa kwa uchaguzi kwa nafasi ya Mwenyekiti.

UJUMBE KWA FACEBOOK