TTCL

Habari

CCM WATAKIWA KUUNDA KAMATI ZA MAADILI

on

Mwenyekiti wa CCM Mbeya mjini Affrey Nsomba akisalimia wajumbe wa kikao cha Sekretarieti ya CCM kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Mbeya.Katibu wa CCM Mbeya mjini (Katikati) Gerald Mwadalu akiongoza kikao cha Sekretarieti ya CCM kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mbeya day sekondariBaadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wanaotokana na Chama cha Mapinduzi wakitambulishwa katika kikao cha Sekretarieti ya CCM Mbeya mjini hivi karibuniBaadhi ya Wajumbe  wa Sekretarieti ya CCM Mbeya mjini wakiwa kwenye kikaoWajumbe  wa Sekretarieti ya CCM Mbeya mjini wakiwa kwenye kikao

 

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya mjini kimetakiwa kuunda kamati ya nidhamu kuanzia ngazi ya Matawi, Kata na Wilaya ili kushughulikia mienendo mibovu ya Wanachama na viongozi.

 

Rai hiyo ilitolewa juzi na Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya mjini, Gerald Mwadallu wakati wa kikao cha maelekezo kwa wajumbe wa Sekretarieti ya Wilaya hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Mbeya.

 

Mwadallu alisema agizo hilo linapaswa kutekelezwa haraka kutokana na maelekezo ya Katiba mpya na Kanuni za CCM ambazo zinataka uwepo wa Kamati ya maadili kuanzia ngazi ya Tawi, Kata hadi Wilaya.

 

Alisema kamati hiyo itasaidia kujadili na kurekebisha na kusuluhisha mienendo mibaya na utovu wa nidhamu wa baadhi ya wanachama pamoja na viongozi.

 

Aliongeza kuwa Kamati hiyo inaundwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ambapo Mwenyekiti na Katibu wanakuwa wajumbe pamoja na wajumbe wengine watatu kutoka Kamati ya siasa.

 

Alisema wajumbe wa kamati ya siasa watatu watapigiwa kura ya siri kwa kuzingatia jinsi ili kukamilisha idadi ya wajumbe watano wanaounda kamati ya maadili.

 

Mwadallu alisema kipindi cha uchaguzi kimepita lakini kinakuwa na mambo mengi ikiwemo makundi na malalamiko mengi hivyo hayana budi kuisha ili kazi za Chama ziweze kusonga mbele.

 

Alisema kwa mujibu wa Katibu suala la makundi wakati wa uchaguzi ni haki ya kila mwanachama ila baada ya kutangazwa washindi makundi yote huvunjwa hivyo wanaoendeleza hadi sasa ni watovu wa nidhamu.

 

Naye Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Mbeya mjini, Philimon Mng’ong’o alisema baada ya uchaguzi viongozi wote kuanzia ngazi za matawi wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia mambo matatu.

 

Aliyataja mambo hayo kuwa ni kufanya kazi kwa kutumia akili nyingi, kufanya kazi kwa uvumilivu mkubwa pamoja na kufanyakazi kwa kasi ya ajabu ili kuweza kukomboa Mitaa na Kata katika uchaguzi wa mwakani.

 

Hata hivyo katika kikao hicho pia wajumbe walipokea ripoti ya uchunguzi iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na timu yake katika kubaini mali za Chama cha Mapinduzi zilizouzwa, zinazotaka kuporwa kinyemela.

 

Aidha katika ripoti hiyo ilibaini uwepo wa migogoro saba katika Kata za Ilemi,Ruanda,Manga,Itezi na Ilomba ambapo kuna uvamizi wa maeneo ya Chama uliofanywa na watu binafsi pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

 

Mwisho.

UJUMBE KWA FACEBOOK