TTCL

Habari

CWT KYELA WATAKA UPENDELEO MADAI YA WALIMU

on

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya CWT Taifa,Lusajo Mwambola akifungua mkutano wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kyela uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Kyela Pollytechnic. Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT)Wilaya ya Kyela Mwalimu Lwitiko Mwaseba akizungumza jambo katika mkutano wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kyela ambapo wameiomba Serikali kutoa kipaumbele cha Kulipa Watumishi kwa kuanza na WalimuViongozi wa Chama cha Walimu wakiwaongoza Walimu kuimba wimbo wa mshikamano kabla ya kuanza kwa mkutano wao Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Walimu Wilaya ya Kyela wakifuatilia kwa makini mkutano wa Chama hicho uliofanyika kwatika ukumbi wa Chuo cha Kyela Pollytechnic.

 

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kyela kimeitaka Serikali kutoa kipaumbele kwa Walimu pindi watakapoanza kulipa madeni ya watumishi wa umma.

Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Wanachama wa Chama cha Walimu wakati wa Mkutano mkuu wao uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Kyela Polytechininc.

Wakizungumza katika mkutano huo Walimu Lucia Lyanzi na Mwalimu Azizi Ng’ambage walisema Serikali ya awamu ya Tano imejitahidi kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato sambamba na ukusanyaji wa fedha hivyo watakapoanza kulipa madeni waanze na walimu.

Walisema Walimu ndiyo kada inayotegemewa katika kuzalisha watumishi katika sekta mbalimbali nchini hivyo ili kuendelea kupata wataalam ni vema Walimu wakatazamwa kwa jicho la pekee.

Waliongeza kuwa madeni ya Walimu ni madogo ambayo yanalipika kirahisi ikiwemo malimbikizo ya mishahara, kutokupewa stahiki zao za kupandishwa madaraja, fedha za uhamisho na marupurupu mbalimbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Kyela, Mwalimu Aliko Mwaseba alisema Serikali inapaswa kukithamini chama cha Walimu kwa kuwa ndicho chama kinachowasemea Watumishi wote.

Alisema Licha ya kuwepo kwa Vyama vya Wafanyakazi lakini Chama chenye nguvu na kinachoweza kuwasemea watumishi wa umma ni CWT pekee.

Awali akifungua Mkutano huo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CWT Taifa, Mwalimu Lusajo Mwambola alisema Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na imeahidi kulipa madai ya Walimu kwa Wakati.

Aidha aliwasihi Walimu kuwa wavumilivu na kutimiza Wajibu wao wa kufundisha katika kipindi ambacho wanasubiri kulipwa stahiki zao.

Alisema kwa mujibu wa ajira kazi ya Mwalimu ni kuhakikisha wanafundisha na kufaulisha wanafunzi hivyo ni vema wakatimiza jukumu hilo kwa weledi mkubwa bila kujali madai wa;liyonayo kwani Serikali imeahidi kuanza kulipa.

UJUMBE KWA FACEBOOK