TTCL

Makala

ELITREA: WANAUME WAPEWA AGIZO LA KUOA MKE ZAIDI YA MMOJA, KIFUNGO CHA MAISHA KUWAKABILI WATAKAOPUUZA

on

Wanaume nchini Elitrea wamepewa amri ya kuoa angalau wake wawili au zaidi kwa kila mwanaume huku adhabu ya kifungo cha maisha jela kutolewa kwa atakaekaidi amri hiyo ya serikali.

Kwa mujibu wa serikali agizo hilo limetolewa kufuatia uwepo wa idadi ndogo ya wanaume ikilinganishwa na idadi ya wanawake ikiwa ni matokeo ya vita kati ya taifa hilo na Ethiopia.

Serikali nchini humo imewathibitishia raia wake kuwa itagharamia sherehe za harusi na nyumba kwa wanandoa

Kwa mujibu wa tovuti ya Afkinsider.com  iliyochapisha taarifa hiyo, Onyo limetolewa kwa mwanamke au mwanaume atakaekaidi agizo hilo atahukumiwa kifungo cha maisha jela na kazi ngumu.

Zaidi ya wanajeshi 150,000 wa Eritrea waliuawa kwenye vita huko Ethiopia kati ya mwaka 1998 hadi 2000

UJUMBE KWA FACEBOOK