TTCL

Habari

EPICOR 10.2 KUPUNGUZA HOJA ZA CAG KWA HALMASHAURI NCHINI

on

Mkurugenzi msaidizi Shughuliza Serikali Ofisi ya Rais Tamisemi, Johnson Nyingi akitoa hotuba ya kufungua mafunzo ya mfumo mpya wa Epicor 10.2 kwa Maafisa ugavi kutoka Halmashauri za Mikoa ya Mbeya, Songwe,Njombe, Katavi na Rukwa yanayofanyika jijini Mbeya. Afisa Usimamizi wa fedha kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mmaka Mwinjaka akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo kwa Maafisa Ugavi. Maafisa Ugavi wakiwa katika chumba cha mafunzo ya mfumo mpya wa Epicor 10.2 yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Usungilo jijini Mbeya Maafisa Ugavi wakifuatilia kwa makini mafunzo katika ukumbi wa Usungilo jijini Mbeya Washiriki wa mafunzo ya Epicor 10.2 kwa maafisa ugavi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi msaidizi Shughuli za Serikali  Tamisemi baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo

 

MAAFISA Ugavi, Wahasibu na Watunza hazina wa Halmashauri nchini wametakiwa kutumia vizuri taaluma zao katika kutatua changamoto za vituo vyao vya kazi hususani hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu serikalini (CAG).

Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi msaidizi shughuli za Serikali Ofisi ya Rais Tamisemi, Johnson Nyingi alipokuwa akifunga mafunzo ya mfumo mpya wa Epicor 10.2 kwa Wahasibu na Watunza hazina na kufungua mafunzo ya Maafisa ununuzi wa Halmashauri za Mikoa ya Mbeya,Njombe,Songwe, Katavi na Rukwa yanayofanyika jijini Mbeya.

Mafunzo hayo yanatolewa kwa msaada wa Uimarishaji wa mifumo ya sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa shirika la misaadfa la Marekani (USAID).

Mkurugenzi huyo alisema mategemeo ya Serikali na wadau ni kuona mabadiliko baada ya wataalam kupata mafunzo hususani katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha.

Alisema hoja nyingi za mkaguzi zinatokana na hesabu za Halmashauri kutokukaa vizuri jambo linalosababishwa na kukosekana umakini kwa wataalamu ambao ni maafisa ugavi, wahasibu na Watunza hazina.

Alisema kazi za Watunza hazina, Maafisa ugavi na wahasibu ni kutoa ushauri kwa Wakurugenzi na watoa huduma wao ili kufuata taratibu za fedha zinavyotakiwa.

Aliongeza kuwa matarajio ya Serikali ni kuona malipo mbalimbali ndani ya Halmashauri yanalipwa kulingana na bajeti iliyopo na taratibu zilizopo.

“Taarifa ya ukaguzi huja mbaya licha ya bajeti kukaa vizuri lakini tatizo linakuja kuonekana kwenye mahesabu ya matumizi ya fedha kuwa na kasoro na hiyo kazi hufanywa nawatunza hazina pamoja na wahasibu hivyo mkarekebishe na kutoa majibu ya hoja hizo” alisema Mkurugenzi.

Kwa upande wake Mweka hazina kutoka Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Amede Ng’wanidako akishukuru kwa niaba ya washiriki wa mafunzo aliipongeza Serikali kwa kuwapatia mafunzo yaliyowaongezea ufanisi katika majukumu yao.

Aidha alitoa wito kwa washiriki wenzie kutumia elimu waliyoipata kufundisha wengine ikiwa ni pamoja na kujibu maswali kutoka kwa wadau wao yanayotokana na ufanisi wa mfumo mpya wa Epicor 10.2

UJUMBE KWA FACEBOOK