TTCL

Habari

FORTUNATUS KASOMFI AZIKUMBUKA SHULE ALIZOWAHI KUSOMA

on

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sisimba, Rebeka Tindwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea msaada wa sare za mpira wa miguu kwa ajili ya wanafunzi kutoka kwa Fortunatus Kasomfi ambaye alihitimu shule hiyo mwaka 1991.Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sisimba, Rebeka Tindwa akipokea Mpira wa miguu kwa ajili ya wanafunzi kutoka kwa Fortunatus Kasomfi ambaye alihitimu shule hiyo mwaka 1991. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sisimba, Rebeka Tindwa akionesha jezi  baada ya kupokea msaada kutoka kwa Fortunatus Kasomfi ambaye alihitimu shule hiyo mwaka 1991. Fortunatus Kasomfi akionesha mazingaombwe kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Sisimba. Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sisimba wakimsikiliza Fortunatus Kasomfi alipowatembelea Fortunatus Kasomfi akimkabidhi jezi ya Mpira wa miguu kiongozi wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya. Fortunatus Kasomfi akimkabidhi Mpira wa miguu kiranja mkuu  wa Shule ya Sekondari ya Mbeya. Fortunatus Kasomfi akizungumza na wanafunzi wa  Shule ya Sekondari ya Mbeya. Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbeya, Magreth Haule akizungumza baada ya kupokea Mpira na Jezi kwa ajili ya timu ya Shule kutoka kwa Fortunatus Kasomfi ambaye amewahi kusoma shule hiyo Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya wakimsikiliza Fortunatus Kasomfi Fortunatus Kasomfi akiangalia moja ya michoro ambayo walikuwa wakifundishwa kuchora katika moja ya darasa la Shule ya Sekondari ya Mbeya. Kikosi cha Kampuni ya The Mbongobongo kikiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na Walimu ya Shule ya Msingi Sisimba Fortunatus Kasomfi akikumbushia namna alivyokuwa akikaa golini katika uwanja wa mpira wa  Shule ya Sekondari ya Mbeya.

 

WATANZANIA wametakiwa kuwa na utamaduni wa kurudisha fadhila kwa jamii na taasisi zilizowawezesha kupata mafanikio katika Nyanja mbalimbali.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya, Magreth Haule pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sisimba, Rebeka Tindwa zilizopo jijini Mbeya.

Walimu hao walitoa wito huo walipokuwa wakipokea msaada wa Mipira pamoja na sare za mpira wa miguu kutoka kwa Mwanafunzi ambaye aliwahi kusoma shule hizo miaka ya nyumba Fortunatus Kasomfi anayeishi nchini Afrika kusini.

Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Sisimba, Rebeka Tindwa alisema ni mara chache kutokea kwa watu waliopata mafanikio kukumbuka walikotoka na kutoa msaada.

“Ni watu wachache kuwakumbuka waliowasaidia kupata mafanikio na kuwatembelea ili kuwashukuru hivyo tunamshukuru huyu kijana kwani alihitimu hapa mwaka 1991 hivyo wengine waige mfano wake” alisema Mwalimu huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya kutwa Mbeya, Magreth Haule alisema kama kila aliyepita katika shule hiyo akajitokeza kutoa ushuhuda wa mafanikio yake kutasaidia kuongeza hamasa kwa wanafunzi waliopo mashuleni.

Alisema wanafunzi wa siku hizi wamekuwa na tabia mbaya ikiwemo utoro na uchelewaji wa kufika Shule hivyo wahitimu waliofanikiwa wakitoa ushuhuda mbele yao kutasaidia kuwabadilisha.

Hata hivyo kwa pamoja Walimu hao walitoa wito kwa watanzania wenye mapenzi mema hususani waliosoma katika shule hizo kujitokeza kusaidia kutata changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Walizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na uchakavu wa majengo kutokana na shule hizo kujengwa zamani ambapo Sisimba ilijengwa mwaka 1950 na Mbeya sekondari ikijengwa mwaka 1962.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo, Fortunatus Kasomfi alisema baada ya kupata mafanikio katika shughuli zake nchini Afrika kusini amekumbuka chimbuko lake kuwa ni shule alizosoma.

Alisema ameona kutoa vifaa vya michezo kutokana na kupenda mpra wa miguu ambapo akiwa mwanafunzi alizitumikia timu za shule kwa mafanikio.

Alisema kwa kuanzia ameona atoe seti moja moja kwa kila shule sambamba na mpira ili wengine waweze kuguswa kwa kuchangia kutatua changamoto ya uchakavu wa majengo.

Aliongeza kuwa katika mafankio yake ambayo yametokana na msingi mzuri kutoka kwa Walimu wa Shule ya Msingi Sisimba na Sekondari ya Mbeya hivi sasa anajishughulisha na kazi za sanaa pamoja na ujasiliamali.

 

 

UJUMBE KWA FACEBOOK