TTCL

Habari

GEITA WAPONGEZA HUDUMA ZA NHIF

on

aHospitali Teule ya mkoa wa Geita ambambo mpango huo unaendeshwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

za huduma za madaktari bingwa.

KaimuMkurugenziwaHudumazaMatibabunaUshauriwaKitaalam Dk. AifenaMrambaambayealimwakilishaKaimuMkurugenziMkuuwa NHIF, BenrardKonga,akitoamaelezoyaawalikwenyeuzinduziwahudumahizo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Selestine Gesimba akihutubia wananchi waliofika katika,uzinduzi huo.

Mramba akikabidhi Mashuka na Vifaa tiba kwa uongozi w aMkoa wa Geita kwa ajili ya matumizi ya zoezi la Madaktari Bingwa.

Wananchi wenye uhitaji wahuduma za Kibingwa wakiwa kwenye mstari wa kuandikishwa

Na Grace Michael, Geita

Mamia ya wananchi mkoa ni Geita wamejitokeza kupata huduma za madaktari  bingwa , mpango unaotekelezwa kwa ushiriiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mpango huo ulianza kutekelezwa siku ya Jumatatu  wiki  hii, katika mikoa ya Geita na Kigoma unaolenga kuwahudumia wagonjwa ambao wanahitaji huduma za kibingwa ambazo hazipo katika Hospitali hizo.

Madaktari bingwa wanaoshiriki katika mpango huo ni wa magonjwa ya watoto, mfumo wa mkojo,  magonjwa ya ndani na moyo,  magonjwa ya pua, masikio na koo pamoja na huduma za dawa za usingizi na huduma za wagonjwa mahututi.

Wakizungumza katika uzinduzi wa mpango huo uliofanyika katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa Geita, wananchi waliojitokeza kupata huduma Hizo wamesema ujio wa wataalamu hao umekuwa msaada mkubwa na umewaondolea usumbufu na gharama kubwa ambazo wa ngelazimika kuzitumia kufuata huduma hizo nje ya mkoa wao.

Mfuko umetenda jambo jema sana naunapaswa kupongezwa hasa kwa kuona umuhimu wa kusogeza huduma hizi karibu na wananchi wengi wenye mahitaji kwa mfano mimi ni mjane hapa nilipo lakini mpango huu umeniwezesha kuwaona hawa wataalam ambao kwa hali ya kawaida nisingewao na hivyo napongeza Mfuko wa Serikali yetu inayoongozwa na Dk. Pombe John Magufuli,..” Alisema Bi. Leah Ezekiel.

Akito amaelezo ya awali Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya , Dk. Aifena Mramba alisema kuwa kwamu dawa siku mbili za zoezi hilo katika mikioa ya Kigoma na Geita,  jumla ya wagonjwa  1,204, wameonwa na kuhudumiwa na madaktari bingwa.

Alisema kwaidadi hiyo imetoa taswira ya mahitaji ya wananchi katika huduma za kibingwa jambo linalotoa hamasa kwa Mfuko kuangalia namna ya kuendesha program hizo katika maeneo mengi zaidi.

“…Kwa madaktari tuliowaleta, wametuhakikishia kuwa wakotayari kufanyakazi kwa muda wowote iliwagonjwa wote waliofika kwa ajili ya mpango huo wa huduma iwe na mfano mzuri jana kuna madaktari waliofanya kazi hadi saa sita usiku…”alisema Dk. Mramba.

KatibuTawala wa Mkoa wa Geita Selestine Gesimba, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa katika uzinduzi wa mpango huo, ameomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuangalia namna ya kufanya huduma hizi kuwaendelevu kwa kuwazimeonyesha mafanikio makubwa katika kuwahudumia wananchi ambao uwezo wao ni mdogo kufuata huduma mbali.

Aliviagiza vituo vya matibabu mkoani humo kuendelea kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika fursa mbalimbali zinazolenga kuboresha huduma ikiwa nipamoja na kutumia fursa ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo ili kuboresha huduma katika vituo vyao.

Aidha amewahimiza wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii ili kujihakikishia upatikanaji wa kupatahuduma kwa kuchangia kabla ya kuugua na kuepukana na usumbufu wa kutafuta fedha za matibabu wakatiwanapougua.

Mwisho.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK