TTCL

Makala

Je  wajua kiwanda bora cha kutengeneza bia barani Afrika kipo Mbeya nchini Tanzania? 

on

Wafanyakazi wa Kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na kombe na cheti cha ushindi baada ya kiwanda hicho kutwaa tuzo ya kuwa kiwanda bora  na kushika nafasi ya kwanza Afrika kati ya viwanda 21 vya bia barani Afrika muda mfupi baada ya Meneja wa Kiwanda hicho, Jemedari Waziri kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA)-Mbeya akitokea Afrika ya Kusini.

Wafanyakazi wa  kiwanda  cha Bia cha TBL- Mbeya, wakionyesha kombe na cheti cha ushindi mitaani  wakati wa mapokezi ya Meneja wa Kiwanda hicho.

 Meneja Rasilimali watu wa kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, Sarah Zayumba (aliyeshika kombe), akiwa ameshika kombe  hilo baada ya kuwasili katika kiwanda hicho.

Kombe la Ushindi ambalo  kiwanda kimetunukiwa

Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya wakiangalia kombe la ushindi

Baadhi ya wafanyakazi wakipata chakula katika hafla ya kusheherekea ushindi

Wakati serikali ya awamu ya tano ikiweka mikakati ya kuifanya Tanzania nchi ya viwanda tayari dalili njema zimeishajitokeza kuwa tukiamua tunaweza kwa kuwa kiwanda kinachoshikilia rekodi ya ubora barani Afrika ni kiwanda cha kutengeneza bia cha TBL kilichopo katika kitongoji cha Iyunga  ndani ya Jiji la Mbeya.

 

Kwa mara nyingine,  baada ya kushindanishwa na  viwanda vikubwa vipatavyo 21 barani Afrika, mwishoni mwa wiki iliyopita TBL Mbeya imeibuka kinara na kutangazwa kuwa kiwanda bora barani Afrika kati ya viwanda vilivyopo chini ya kampuni kubwa yenye viwanda vya kutengeneza bia ya SABMiller na kulinda rekodi yake ya kuwa kiwanda bora.

 

Rekodi hii inadhihirisha kuwa uwekezaji wa viwanda sio lazima ufanywe maeneo ya mijini kama ambavyo ilikuwa imezoeleka kwa muda mrefu.

 

Akiuzngumzia ushindi huo Meneja wa Kiwanda hicho, Mhandisi Jemedari Waziri, alisema anajivunia ushindi huo kwani uthibitisho halisi kuwa watanzania tunaweza kufanya vizuri  na kuleta maendeleo kwa kasi tukiamua.

 

“Tunaposema ubora wa kiwanda tunaamaanisha ubora wa bidhaa tunazozalisha, teknolojia tunazotumia, raslimali watu tuliyonayo, mchango wa kiwanda kwa Serikali na jamii iliyotuzunguka bila kusahau utunzaji wa mazingira ambayo ni moja ya nguzo ya kampuni yetu”.Alisema.

 

 

 

Aliongeza kuwa ushindi huu ni kwa wana Mbeya wote na wana kanda ya Nyanda za Juu Kusini “Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kutuunga mkono  wakati wote na tutaendelea kuwaletea bidhaa bora kwenye soko na kubuni miradi mbalimbali ya kijamii itakayosaidia kuleta mabadiliko”.Alisema

 

Jemedari pia alisema ushindi huu unatokana na jitihada za pamoja kutoka kwa wafanyakazi wote wa kiwanda na TBL Group kwa jumla na anafurahi kuona kiwanda kinaendeshwa na watanzania asilimia kubwa ikiwa ni vijana waliobobea katika fani mbalimbali.

UJUMBE KWA FACEBOOK