TTCL

Habari

Kiboko ajeruhi mtu mmoja, auawa kwa risasi  na maafisa wa wanyamapori.

on

Mnyama aina ya kiboko amezua taharuki kubwa katika kijiji cha Ijumbi Kata ya Ruiwa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya baada ya kumjeruhi vibaya Damas Kyando mkono, tumbo na makalio.

 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Ijumbi Mugabe Sumuni amesema tukio limetokea asubuhi mei 18 mwaka huu wakiwa wawili wakienda shamba ndipo alipotokea kiboko huyo katika hali ya kujihami majeruhi alipiga shoka mgongoni ndipo kiboko alitaharuki na kukanyaga mkono na kumuuma tumbo na makalio. Baada ya kupiga yowe wananchi waliojitokeza kujaribu kumshambulia kwa mawe bila mafanikio ndipo Askari wanyamapori walifika na kumpiga risasi nane hadi kufa

Na Ezekiel Kamanga Mbarali

UJUMBE KWA FACEBOOK