TTCL

Habari

KITULO, HIFADHI YA TAIFA YENYE SIFA ZA KIPEKEE DUNIANI.

on

Wanachama wa TAJATI wakiwa katika majumuisho baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Kitulo WanaTAJATI wakiwa kwenye maporomoko ya Maji ya Mwakipembo ndani ya Hifadhi ya Taifa Kitulo WanaTAJATI wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kitulo  WanaTAJATI wakifurahia mandhari mazuri ndani ya Hifadhi ya Taifa ya KituloNdege aina ya Korongo mweupe wanaohama kutoka Kaskazini mwa Bara la Ulaya akiwa ndani ya Hifadhi ya Kitulo kama alivyokutwa wakati wa ziara ya TAJATI. Mandhari ya kupendeza ya Hifadhi ya Taifa ya Kitulo inayofananishwa na Bustani ya Eden Moja  kati  ya aina 40 za maua yanayopatikana katika Hifadhi ya Taifa KituloAlama ambayo ilikutwa kwenye mmoja ya Ndege wanaohama inayoonesha alitokea nchini Poland.

WADAU wa Utalii kutoka nje na ndani ya Nchi wanakaribishwa kuwekeza na kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Kitulo kujionea vivutio mbalimbali.

Rai hiyo ilitolewa na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) walipotembelea Hifadhi hiyo mwishoni mwa wiki.

Wakiwa ndani ya Hifadhi hiyo iliyopo katika Mikoa ya Mbeya kwa wilaya za Rungwe na Mbeya pamoja na Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Wanachama hao walishuhudia ndege aina ya Korongo Mayobwe na Korongo mweupe.

Akizungumzia sifa ya ndege hao, Muikolojia kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kitulo, Frank Mapunda alisema ndege hao hufika Kitulo kwa ajili ya mapunziko wakitokea Ulaya kaskazini kuelekea Afrika ya kusini.

Alisema ndege hao huwasili katika Hifadhi ya Kitulo kuanzia mwezi Novemba hadi Aprili kipindi ambacho hukimbia baridi kali nchini kwao.

Alisema sababu ya ndege hao kwa makundi makubwa kutua katika Hifadhi ya Kitulo ni kutokana na kupendelea kukaa kwenye ukanda wa wazi wenye miti mifupi ambapo Kitulo inayosifa hiyo pamoja na uwepo wa Viwazi jeshi kwa wingi ambacho ni chakula kikuu cha ndege hao.

Aliongeza kuwa hivi karibuni mmoja wa ndege alikufa katika hifadhi ya Kitulo kutokana na kuugua lakini baada ya kumchunguza ilibainika alikuwa amevalishwa ringi kama kitambulisho kikionesha ndege huyo anafanyiwa utafiti na Shirika la Utafiti wa ndege la Polland.

Naye Afisa Utalii mwandamizi katika Hifadhi ya Kitulo, Eva Pwele alisema pamoja na Kitulo kuwa na sifa ya kupokea ndege wahamao lakini bado mwitikio wa watalii wa ndani na Nje ya Nchi ni mdogo.

Alisema katika kipindi cha kuanzia mwezi Novemba hadi Aprili licha ya kuwepo kwa ndege hao pia ni kipindi ambacho maua zaidi ya aina 40 yanayopatikana Kitulo pekee yanakuwa yamestawi.

Alisema katika kipindi hicho kunakuwa na Watalii kati ya 40 hadi 60 ikiwa ni wastani wa Watalii 45 jambo ambalo linaonesha mwitikio kuwa mdogo.

Wakizungumzia fursa za utalii na Uwekezaji uliopo ndani ya Hifadhi hiyo, Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka Mwakilili alisema ni vema Watanzania na wageni wakajitokeza kuwekeza kwenye miundombinu hususani kwenye ujenzi wa maeneo ya kupumzikia watalii.

Naye Mkurugenzi wa Habari na mahusiano wa TAJATI, Felix Mwakyembe alisema ndani ya Hifadhi kuna fursa nyingi za kiutalii na Uwekezaji kama vile Utalii wa Maputo, kutembea kwa farasi, mashindano ya pikipiki na Baiskeli.

Kwa upande wake Mwanachama wa TAJATI, Lukas Malangalila alisema Hifadhi ya Kitulo inapaswa kutiliwa mkazo katika matangazo kwa ni zaidi ya bustani ya Eden.

Alisema endapo matangazo yatatolewa kwa wingi mwitikio wa Watalii zikiwemo Taasisi za umma, mashule na Mashirika binafsi yataanza kutembelea kujifunza na kufurahia mandhari ya Hifadhi.

UJUMBE KWA FACEBOOK