TTCL

Habari

KITUO CHA UTAFITI CHA NIMR – MMRC CHAPONGEZWA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.

on

 

Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyika Kimkoa katika viwanja vya Shule ya Msingi Makongolosi iliyopo Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya Mratibu wa Tafiti na Chanjo kutoka MMRC, Dk. Emmanuel Kapesa akielezea namna kituo na maabara inayotembea ilivyoweza kufanya zoezi la upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa hiari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani ambayo kwa Mkoa wa Mbeya ilifanyika Makongolosi wilayani Chunya. Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk.Yahya Msuya akielezea malengo ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani  ambayo kwa Mkoa wa Mbeya ilifanyika Makongolosi wilayani ChunyaMwenyekiti wa watu wanaoishi na maambukizi ya Ukimwi Mkoa wa Mbeya, Deogratius Kisunga akitoa ushuhuda kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kwa Mkoa wa Mbeya ilifanyika Makongolosi wilayani Chunya Angelina Mchome akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkazi wa WRP- Tanzania kuhusu WRP ilivyoendesha zoezi la nyumba kwa nyumba kupima virusi vya Ukimwi kwenye wiki la Ukimwi duniani ambayo kwa Mkoa wa Mbeya ilifanyika Makongolosi wilayani Chunya Wafanyakazi wa Maabara inayotembea ya MMRC wakimsikiliza mmoja wa mwananchi aliyejitokeza kupata huduma ya upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa hiari siku ya Ukimwi duniani Mwananchi ambaye hakufahamika jina lake mara moja akichukuliwa damu kwa ajili ya kupimwa kama ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwenye Maabara inayotembea ya MMRC Mwenyekiti wa watu wanaoishi na maambukizi ya Ukimwi Mkoa wa Mbeya, Deogratius Kisunga akiwasha mishumaa pamoja na Wakuu wa Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Willium Ntinika (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kwa Mkoa wa Mbeya ilifanyika Makongolosi wilayani Chunya Mtumishi wa Maabara inayotembea ya MMRC, Aza Kamendu akimpa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa baada ya kuitembelea kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyika kimkoa Makongolosi Wilayani Chunya. Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akisikiliza maelezo kutoka kwa wadau wa mapambano ya Ukimwi waliojitokeza kutoa huduma katika viwanja vya shule ya Msingi Makongolosi ambapo maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yalifanyika hapo  Baadhi ya Wakazi wa Makongolosi Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wakipatiwa huduma ya upimaji wa Maambukizi na ushauri nasaha katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani  Viongozi meza kuu wakipiga makofi huku wakiwa wamesimama baada ya kupokea maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyika kimkoa Makongolosi wilayani Chunya mkoa wa Mbeya Baadhi ya Washiriki katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyika Makongolosi wilayani Chunya wakiwa kwenye maandamano Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha Utafiti cha MMRC wakijadiliana jambo katika viwanja vya shule ya msingi Makongolosi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyikaKimkoa katika Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya. Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha Utafiti cha MMRC wakiwa kwenye picha ya pamoja  katika viwanja vya shule ya msingi Makongolosi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyikaKimkoa katika Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya. Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha Utafiti cha MMRC wakifurahia picha ya pamoja katika eneo la kupigia picha lililopo Wilaya ya Mbeya barabara ya Chunya ambapo kwa nyuma kuna bonde la Usangu Wilaya ya Mbarali. Wakazi wa Mji mdogo wa Makongolosi Wilaya ya Chunya wakifuatilia maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo Kimkoa yalifanyika Chunya.

KITUO cha utafiti wa magonjwa na Chanjo (MMRC) kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda jijini Mbeya kimepongezwa kwa jitihada zake katika mapambano dhidi ya Ukimwi.

 

Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Disemba Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika viwanja vya Shule ya Msingi Makongolosi wilayani Chunya.

 

Aidha katika maadhimisho hayo, Mkuu huyo wa Wilaya alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

 

Katika hotuba yake hiyo, Madusa alisema katika mapambano dhidi ya Ukimwi wadau mbalimbali wanapaswa kushirikiana na Serikali hivyo jitihada zinazofanywa na kituo cha utafiti cha MMRC zinapaswa kuungwa mkono.

 

Aidha alitoa wito kwa mashirika mengine kama WRP Tanzania, Kihumbe kuendelea na jitihada za kuhakikisha kauli mbiu ya Tanzania bila Ukimwi inawezekana kwa kufanya kwa vitendo.

 

Madusa pia alisema Mbeya imejipanga kuhakikisha inatokomeza maambukizi ya Ukimwi kwa kuendelea kushirikiana na wadau katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi na madhara ya ugonjwa wa Ukimwi.

 

Alisema mkakati mwingine ni kuendelea kutoa ushauri nasaha kwa jamii, kuhamasisha tohara kwa wanaume, upimaji wa hiari, matumizi sahihi ya Kondomu pamoja na jitihada za kuzuia maambukizi ya mama mjamzito kwenda kwa mtoto anayezaliwa.

 

Naye Mratibu wa Tafiti na Chanjo wa MMRC,Dk.Emmanuel Kapesa kwa niaba ya Mkurugenzi alisema hadi sasa dawa ya Ukimwi haijapatikana hivyo kote duniani tafiti zinaendelea ili kupata tiba yake.

 

Alisema zaidi kilichopatikana sasa ni dawa za kufubaza makali ya Ugonjwa wa Ukimwi lakini kinachoendelea kwa sasa ni kutafuta chanjo ya Ukimwi kwa maana Kinga ni bora kuliko tiba.

 

Kwa upande wake Msimamizi wa Maabara inayotembea inayomilikiwa na Kituo cha utafiti wa magonjwa MMRC, Dk. Wiston William alisema katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani maabara hiyo imetoa huduma za upimaji wa virusi na magonjwa mengine katika maeneo ambayo yalikuwa hayafikiki kirahisi.

 

Akitoa ushuhuda mbele ya hadhara Mwenyekiti wa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Mkoa wa Mbeya, Deogratius Kisunga alisema pamoja na kuishi na maambukizi kwa miaka 24 lakini hajateteleka kiafya kutokana na kufuata maelekezo ya Wataalam wa afya.

 

Aidha alitoa wito kwa Watanzania wote kushirikiana na Serikali pamoja na wadau kuhakikisha mapambano dhidi ya Ukimwi yanafanikiwa kwa kila mtu kuchukua tahadhari katika kuhakikisha malengo ya 90 tatu na sifuri tatu yanatimia.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK