TTCL

Habari

MAADHIMISHO YA HIJA YA UTUME WA FATIMA ULIMWENGUNI YAHITIMISHWA KITAIFA JIJINI MBEYA

on

 

Askofu Evaristo Chengula wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya akipokea maandamano ya Mahujaji wa Utume wa Fatima katika Misa iliyofanyika katika Kanisa la Hija Mwanjelwa jijini MbeyaAskofu Evaristo Chengula wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya akiongoza maandamano ya Mahujaji wa Utume wa Fatima katika Misa iliyofanyika katika Kanisa la Hija Mwanjelwa jijini Mbeya Mhashamu Baba Askofu Evaristo Chengula akiwasha mshumaa katika Mnara wa Hijja uliopo katika Kanisa la Hija Mwanjelwa baada ya kuuzindua katika maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 100 tangu Bikira Maria alivyowatokea watoto wa Fatima Nchini Ureno 1917 Mmoja wa Wahujaji, Josephine Kamunga akielezea umuhimu wa Utume kwa Wakristo katika kuondolewa dhambi zao katika maisha ya kila siku Watawa na Wahujaji wakiwa kwenye maandamano ya kuhitimisha maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 ya Bikira Maria kuwatokea watoto wa Fatima nchini Ureno. Mapadre na Masista wakiwa kwenye maandamano ya Hija jijini Mbeya Brass band ya Shule ya Sekondari ya Wasichana St. Francis ikiongoza maandamano ya Mahujaji Mahujaji wakiwa wamefika katika Kanisa la Hija Mwanjelwa kwa ajili ya Ibada ya Misa Waumini mbalimbali wakiwa wameungana na Mahujaji kwenye maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 tangu Bikira Maria alipowatokea watoto wa Fatima nchini Ureno.

 

MAELFU ya Mahujaji   wa Kanisa Katoliki nchini wamekutana katika Misa ya Hija ya Utume wa Fatima kuadhimisha Jubilei ya miaka 100 tangu Mama Bikira Maria alipowatokea watoto watatu wa Fatima nchini Ureno.

Misa hiyo iliyoongozwa na Maaskofu wanne akiwemo Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo la Mbeya, Gervas Nyaisonga wa Jimbo la Mpanda sambamba na Askofu Libena (Ifakara) na Askofu Ngonyani kutoka Lindi ibada iliyoadhimishwa katika Kanisa la Hija Mwanjelwa jijini Mbeya.

Aidha watoto waliotokewa na Bikira Maria 1917 nchini Ureno ni Lucia, Francis na Hyasinta ambao aliwapa ujumbe kwa binadamu kusali Rozari kila wakati ili kujikomboa na dhambi ikiwa ni pamoja na kuwaombea wengine wenye mahitaji mbalimbali.

Akizungumzia Misa hiyo, Mwenyekiti mstaafu wa Wanahija Taifa, Joseph Mtuka alisema kabla ya misa Hija ilitanguliwa na mafunzo kwa washiriki samba mba na kuadhimisha mateso ya Yesu kwa kupanda Mlima Loleza kisha Maandamano yaliyoanzia Kanisa kuu la Mtakatifu Anton wa Padua mjini na Kuishia Kanisa la Hija Mwanjelwa.

Alisema pamoja na kushiriki ibada ya Hija yeye pamoja na Waumini 35 walienda hadi Ureno eneo ambalo  ndiko tukio lilikotokea ambako pia waliungana na Baba Mtakatifu Papa Francis kwa kusali ibada ya Misa pamoja.

Naye Mhujaji Josephine Kamunga alisema katika maadhimisho hayo yaliyoanza Oktoba 10, Mwaka huu Mahujaji walifundishwa namna ya kusali, kuomba,kuishi utume kwa vitendo kwa kumuenzi Bikira Maria jinsi alivyokuwa mnyenyekevu.

Mhujaji Patson Mtambo alisema waumini kutoka Majimbo mbalimbali Bara na Visiwani wamejumuika wakiwemo Mapadri na Masista ambao pia wameshiriki maandamano ya kupanda Mlima Loleza na matembezi ya kutoka Kanisa la Mjini hadi Mwanjelwa.

Hata hivyo akipokea maandamano ya Mahujaji, Askofu wa Jimbo la Mbeya, Evaristo Chengula alitoa Wito kwa mahujaji kutumia Ibada ya Hija ili iweze kuzisaidia jamii katika maeneo yao kuiga mfano wa matendo ya Bikira Maria.

 

 

UJUMBE KWA FACEBOOK