TTCL

Habari

MAAFISA HABARI NA TEHAMA WAPATIWA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI.

on

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Rebecca Kwandu akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa Maafisa Habari na Tehama wa Halmashauri za Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi yanayofanyika jijini Mbeya. Meneja Mradi wa PS3 Mkoa wa Mbeya, Gasper Materu akiwakaribisha Wawezeshaji na washiriki wa mafunzo ya Habari Maafisa Habari na Tehama wa Halmashauri za Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi. Mkurugenzi wa PS3 wa Ofisi za Mikoa, Dk. Conrad Mbuya akielezea malengo ya mafunzo kwa Maafisa Tehama na Habari yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Usungilo jijini Mbeya. Mkuu wa Timu ya Mawasiliano wa PS3, Leah Mwainyekule akielezea malengo ya muongozo wa tovuti za Mikoa na Halmashauri kwa Washiriki wa mafunzo ya Habari kwa Maafisa Habari na Tehama kutoka Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi. Afisa wa PS3, Neema Kimey akiendelea na majukumu ya kuratibu washiriki wa mafunzo ya habari kwa Maafisa Habari na Tehama wa Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi yanayofanyika jijini Mbeya Afisa Habari kutoka Mkoa wa Mwanza, Remija Salvatory ambaye pia ni muwezeshaji akifundisha washiriki namna ya uandishi wa Habari. Baadhi ya Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kwa makini somo linaloendelea

 

MKUU wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Rebecca Kwandu amewaagiza Maafisa Habari na Tehama wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaweka taarifa sahihi na zinazokusudiwa kwenye tovuti za Serikali.

 

Kwandu ametoa agizo hilo leo Aprili 10, mwaka huu wakati akifungua mafunzo ya namna ya kuandika Habari na kuweka kwenye tovuti yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Usungilo iliyopo jijini Mbeya yakiwahusisha Maafisa Habari na Tehama kutoka Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi chini ya Mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma nchini (PS3) kwa ufadhili wa USAID.

 

Amesema Serikali ilizindua Tovuti za Mikoa na Halmashauri mwezi Machi mwaka huu lakini katika ufuatiliaji ikagundulika uwepo wa changamoto mbalimbali za uendeshaji wa Tovuti hizo kutokana na baadhi ya Halmashauri kutokuwa na Maafisa Habari hivyo Maafisa Tehama kushindwa kuandika habari na kuifanya tovuti kuwa hai.

 

Amesema kutokana na hali hiyo Serikali imeona ni vema ikatoa mafunzo ya pamoja kwa Maafisa Habari na Tehama juu ya namna ya kuandika habari na kuziweka kwenye Tovuti ili ziweze kuwasaidia wananchi kupata taarifa zilizokusudiwa na kwa wakati unaostahili.

 

Mkuu huyo wa Mawasiliano amesema matarajio ya Serikali ni kuona Tovuti zinaendeshwa na kuwekwa habari zilizokusudiwa na kwamba Maafisa hao wataendelea kufuatiliwa na kupimwa ambapo mwisho wa siku kutakuwa na tuzo kwa tovuti bora na mbovu kwa Nchi nzima.

 

Naye Mkurugenzi wa Mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma (PS3) wa Ofisi za Mikoa, Dk. Conrad Mbuya amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha wananchi wanashirikishwa katika shughuli zote ikiwa ni kupanga na kutathmini hivyo kupitia tovuti wananchi wanaweza kuwa na uwezo wa kupata taarifa kwa muda wowote.

 

Amesema mradi wa PS3 uko kwa miaka mitano inayoishia mwaka 2020 ikilenga katika maeneo ya Tehama, rasilimali fedha, rasilimali watu, Tafiti tendaji na utawala bora na ushirikishwaji wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

 

 

UJUMBE KWA FACEBOOK