TTCL

Habari

MAAFISA TEHAMA KUSAIDIA MFUMO WA EPICOR 10.2

on

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Tamisemi, Rebecca Kwandu akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa Tehama kutoka Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi na Njombe yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Usungilo jijini Mbeya. Mkuu wa Timu ya Habari na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma (PS3) Leah Mwainyekule akielezea kuhusu Mradi wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Tehama Mkuu wa Timu ya Habari na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma (PS3) Leah Mwainyekule akipongezana na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini  Ofisi ya Rais Tamisem, Rebecca Kwandu baada ya hotuba ya  ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Tehama Mwenyekiti wa darasa akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo ya Epicor 10.2 kwa Maafisa Tehama Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia kwa makini wawezeshaji katika mafunzo yanayofanyika jijini MbeyaMgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Mfumo wa Epicor 10.2 kwa Maafisa Tehama.

 

MAAFISA Tehama wametakiwa kutumia taaluma zao na utaalam wao kuhakikisha mfumo mpya wa fedha Epicor 10.2 unafanya kazi vizuri na kwa ufanisi.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Tamisemi, Rebecca Kwandu wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa Tehama kutoka Halmashauri za Mikoa ya Katavi,Rukwa, Songwe, Mbeya na Songwe yanayofanyika jijini Mbeya.

Kwandu alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha fedha za umma zinatumika vizuri hivyo kuanzisha mfumo utakaoweza kusaidia katika udhibiti na usimamizi wa matumizi yake.

Alisema lengo la mafunzo ni kuwapa uelewa Maafisa Tehama kuhusu mfumo mpya wa Epicor 10.2 tofauti na mifumo iliyokuwepo awali ambayo kila Halmashauri ilikuwa na utaratibu wake hivyo kuondoa ufanisi katika utendaji wake.

Alisema ili mfumo huo mpya uweze kuwa na matokeo mazuri ni vema Maafisa Tehama wakatumia utaalamu wao katika kuendesha mfumo na kuboresha utendaji kazi wao.

Kwa upande wake Mkuu wa timu ya habari na mawasiliano wa Mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya Sekta za umma (PS3), Leah Mwainyekule aliipongeza Ofisi ya Rais Tamisem kwa kutoa ushirikiano katika kufanikisha shughuli za Mradi.

Alisema Mradi ulilenga Mikoa 13 ya Tanzania Bara lakini kutokana na ushirikiano mzuri kutoka serikalini Halmashauri zote zimenufaika na mifumo hiyo.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK