TTCL

Habari

MADAKTARI RUFAA MBEYA WAPONGEZA UPASUAJI WA NJIA YA MATUNDU

on

Daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na Watoto wa Hospitaliya Rufaa ya Kanda ya Mbeya na Mkuu wa kitengo cha Wazazi Meta, Dk. John Francis akifafanua umuhimu wa upasuaji wa njia ya matundu baada ya kukamilisha zoezi hilo

Msimamizi wa huduma ya upasuaji wa njia ya matundu, Dk. Marc Briere kutoka nchini Marekani akielezea namna madaktari wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya walivyopokea Teknolojia hiyo

Madaktari wakiwa kwenye chumba cha upasuaji wakiendelea kumtibu mgonjwa kwa upasuaji wa njia ya matundu

Madaktari wakifanya upasuaji wa njia ya matundu

Dk. Francis akiwaongoza madaktari kufanya upasuaji wa njia ya matundu

Baadhi ya madaktari wakifuatilia kwa makini zoezi la upasuaji wa njia ya matundu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.

MADAKTARI bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya wamepongeza teknolojia mpya ya upasuaji kwa njia ya matundu inayofanyika hospitalini hapo.

Akizungumza baada ya kufanya zoezi la upasuaji kwa njia ya matundu kwa wagonjwa mbalimbali, Daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi na watoto, John Francis ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Hospitali ya Wazazi Meta alisema teknolojia hiyo inarahisisha utendaji wa kazi kwa madaktari.

Alizitaja faida za upasuaji wa njia za matundu kuwa ni pamoja na kumrahisisha daktari kufanya upasuaji kwa wagonjwa wengi kwani huchukua dakika 40 hadi 60 kwa mgonjwa mmoja.

Alisema faida nyingine mgonjwa hakai muda mrefu hospitali ikiwa ni pamoja na kulazwa kwani baada ya upasuaji anaruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea na shughuli zake.

Alisema pia si rahisi kwa mgonjwa kupatamaambukizi ikiwemo kidonda kutunga usaha kwani upasuaji huo hautengenezi kidonda kikubwa ambapo pia humuokolea gharama na muda wa kutembelewa hospitali na kuletewa vyakula.

Kwa upande wake msimamizi wa huduma hiyo, Dk. Marc Briere kutoka nchini Marekani aliwapongeza madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kwa kuielewa Teknolojia hiyo mapema kwa kuwa ni mpya.

Alisema ameweza kukaa Hospitali hapo kwa muda wa wiki mbili akitoa maelekezo lakini madaktari wameonesha uelewa mapema na kuanza kuzitumia kufanya upasuaji kwa wagonjwa.

UJUMBE KWA FACEBOOK