TTCL

Habari

MADIWANI MBEYA WAPEWA ELIMU YA KUENDESHA HALMASHAURI ZAO

on

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika akifungua mafunzo ya siku mbili kwa madiwani wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya juu ya namna ya kuziendesha Halmashauri zao kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. Mratibu wa Mradi wa PS3 Mkoa wa Mbeya akielezea umuhimu wa mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Madiwani wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya. Mwakilishi wa Chuo cha Serikali za Mitaa za Hombolo Mkoa wa Dodoma Dk. Michael Msendekwa akielezea umuhimu wa Madiwani kupata mafunzo ya uendeshaji wa Halmashauri zao Mwakilishi wa Mradi wa PS3, Dk.Peter Kilima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa madiwani wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika hivi karibuni Baadhi ya Madiwani na Wakurugenzi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo

MADIWANI kote nchini wametakiwa kuwa karibu na wananchi wao kwa kuwashirikisha katika shughuli za maendeleo jambo ambalo litachangia wao kuielewa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania kiurahisi.

Hayo yalibainishwa jana na Mwakilishi wa Mradi wa Mfumo wa uimarishaji wa Sekta za Umma (PS3)  unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani (USAID), Dk. Peter Kilima wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uendeshaji wa Halmashauri kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti na Madiwani wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.

Alisema Madiwani ni wawakilishi na watu wa karibu na wananchi hivyo wakipewa elimu nanma ya kuwashirikisha katika shughuli za maendeleo itasaidia kuwaweka karibu na serikali yao hivyo kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

Aliongeza kuwa mradi huo unaogharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 62 utafanyika kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 na lengo lake ni kuifanya Tanzania kuwa dunia ya pili ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alisema ni muhimu kuwaongezea ujuzi madiwani kwani ndiyo wanaojua matatizo na changamoto zinazowakabili wananchi.

Alisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwani tangu uchaguzi mkuu ufanyike hakuna Diwani aliyepatiwa mafunzo juu ya namna ya kuendesha Halmashauri hivyo hivi sasa Halmashauri zitakuwa na maendeleo baada ya kupata mafunzo.

Aidha alitoa wito kwa Watumishi wa Halmashauri zote kwenda kwenye Chuo cha Serikali za mitaa cha Hombolo mkoani Dodoma ili kuweza kuongeza  maarifa juu ya namna ya kutekeleza majukumu yao jambo litakalochangia kuondoa makosa yanayaotokea.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK