TTCL

Habari

MADIWANI  WA SONGEA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO MOROGORO 

on

KUNDI  la kwanza la waheshimiwa  Madiwani 13  na watalaam watano wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma  limeondoka leo kwa ziara ya mafunzo ya waheshimiwa madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro  ambapo madiwani hao kuanzia Mei 26 hadi 27 mwaka huu,  watajifunza kuhusu ukusanyaji mapato, usimamizi wa taka  na masuala ya  mazingira kwa ujumla.

Kundi la pili la waheshimiwa  Madiwani 15 na watalaam saba linatarajia kufanya ziara ya mafunzo kama hayo katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma  kuanzia Juni 5 hadi 9 mwaka huu. Ziara hizo za mafunzo  zinatarajia kuboresha suala la ukusanyaji wa mapato na suala zima la mazingira.
Na Albano Midelo

UJUMBE KWA FACEBOOK