TTCL

Habari Kwa Picha

MAFUNZO YA TEHAMA YAINGIA SIKU YA PILI MBEYA

on

Mwenyekiti wa timu ya Wawezeshaji wa mafunzo ya uandishi wa Habari kwa Maafisa Habari na Tehama wa Halmashauri za Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi, Athman Pemba ambaye pia ni Afisa Tehama Mkoa wa Tanga akitoa somo la namna ya kufanya mahojiano  Mkuu wa timu ya Mawasiliano wa PS3, Leah Mwainyekule akisimamia uwasilishaji wa kazi za makundi kwa washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari kwa Maafisa Tehama na Habari kutoka Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi. Afisa Teham Mkoa wa Mara, Stephano Amon akifundisha Maafisa Tehama na Maafisa Habari namna ya uandikaji wa habari zinazopaswa kuwekwa kwenye tovuti za Halmashauri zao Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais РTAMISEMI, Rebecca Kwandu akisimamia uwasilishaji wa kazi za makundi kwa washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari kwa Maafisa Tehama na Habari kutoka Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi. Afisa Habari wa Halmashauri ya Musoma, Davis Mafuru akifundisha namna na hatua za uandishi wa habari zinazopaswa kuwekwa kwenye tovuti za Halmashauri katika mafunzo yanayoendelea katika ukumbi wa Hoteli ya Usungilo jijini Mbeya Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandisi wa habari kwa maafisa Tehama na Habari wakiwa ndani ya ukumbi wakifuatilia mafunzo Washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari kwa Maafisa Habari na Maafisa Tehama wa Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayoendelea.

UJUMBE KWA FACEBOOK