TTCL

Habari

MAHAFALI YA 15 YA TIA KAMPASI ZA MBEYA, SINGIDA,MWANZA, NA KIGOMA YAFANYIKA JIJINI MBEYA

on

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Suzana Mkapa akihutubia katika Mahafali ya 15 ya Chuo cha Uhasibu (TIA) kwa Kampasi za Mbeya, Singida, Kigoma na Mwanza yaliyofanyika jijini Mbeya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA)Dk. Joseph Kihanda akitoa taarifa za Taasisi hiyo wakati wa Mahafali ya 15 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika katika Kampasi ya Mbeya  Mwenyekiti wa Bopdi ya Ushauri ya Wizara, Wakili Said Chiguma akitoa hotuba yake kwa wahitimu wa fani mbalimbali wakati wa mahafali ya 15 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania yaliyofanyika katika Kampasi ya Mbeya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Suzana Mkapa akiongoza maandamano wakati wa  Mahafali ya 15 ya Chuo cha Uhasibu (TIA) kwa Kampasi za Mbeya, Singida, Kigoma na Mwanza yaliyofanyika jijini Mbeya Brass band ya Jeshi la Magereza kutoka Kiwira ikiongoza maandamano ya Wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) katika Mahafali ya 15 iliyofanyika katika Kampasi ya MBEYA Wahitimu wa Shahada ya Kwanza ya Manunuzi na ugavi wa Chuo cha Uhasibu Kampasi ya Mbeya wakiwa wamesimama wima wakipokea shahasda yao kutoka kwa mgeni rasmi Wahitimu wa Shahada ya Kwanza ya Uhasibu ya  Chuo cha Uhasibu Kampasi ya Mbeya wakiwa wamesimama wima wakipokea shahada yao kutoka kwa mgeni rasmi Kikundi cha Lizombe kutoka jijini Mbeya kikitoa burudani wakati wa shetrehe za Mahafali ya 15 ya TIA.

 

ZAIDI ya Wahitimu 1800 wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) wametunukiwa Vyeti vya awali, Stashahada, Shahada na Stashahada ya Uzamili katika Fani mbalimbali kwenye Mahafali yaliyofanyika katika Kampasi ya Mbeya kwa mwaka wa masomo 2016/17.

 

Akizungumza katika Mahafali hayo ya 15 ya Taasisi hiyo katika Kampasi za Mbeya, Singida, Mwanza na Kigoma, Afisa Mtendaji mkuu wa TIA, Dkt. Joseph Kihanda alisema kati ya Wahitimu hao Wanawake ni 915 sawa na asilimia 50.3 na Wavulana ni 903 sawa na asilimia 49.7

 

Alizitaja fani za Wahitimu kuwa ni pamoja na Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa biashara,Uongozi wa Rasilimali watu, Masoko na uhusiano wa Umma na Uhasibu wa fedha za umma.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Wizara, Wakili Said Chiguma alitoa wito kwa Wahitimu kwamba elimu waliyoipata ikawe chachu ya mafanikio katika maeneo yao ya kazi watakapoajiriwa na kujiajiri wenyewe.

 

Aliongeza kuwa Elimu waliyoipata ikawe zana au silaha za kuanzia kukabili changamoto watakazokumbana nazo uraiani ikiwemo mabadiliko ya utandawazi na teknolojia hususani kwenye sekta ya ajira.

 

“Napenda niwaase kuwa mtakapokuwa kazini mtumie elimu mliyoipata kuleta mabadiliko ya kweli kwa manufaa yenu nay a waajiri wenu, muoneshe utofauti katika utendaji kazi kati yenu na Wahitimu wa Vyuo vingine ili waajiri wajenge imani kwamba Wahitimu wa TIA ni bora na watofauti hususani katika ubunifu na umahiri” alisema Mwenyekiti.

 

Naye Mgeni rasmi katika Mahafali hayo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Suzana Mkapa aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philipo Mpango alisema ni vema wahitimu wakaendelea na masomo zaidi ili kupata mafanikio katika ngazi za juu.

 

Alisema elimu inayotolewa na TIA imejikita katika masuala ya fedha hivyo ni muhimu katika usimamizi wa mapato ya umma katika kuelekea uchumi wa kati kupitia Viwanda na kwamba Wahitimu waisadie Serikali katika kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanakua kwa manufaa ya Taifa.

 

Aliongeza kuwa Wahitimu wanapaswa kujiimarisha zaidi kiujuzi ili majukumu na kazi zao zisiweze kuchukuliwa na kufanywa na watu wengine kutoka nje ya Nchi kutokana na uwepo wa mabadiliko ya teknolojia ili hali na wao wanaweza kufanya kazi hizo.

 

Naibu Katibu Mkuu  huyo alisema ili kukabiliana na changamoto ya soko la ajira Wahitimu wanapaswa kujikita katika kujiajiri zaidi badala ya kutegemea mfumo rasmi wa Ajira serikalini ambao bado unasumbua.

 

Alitoa wito kwa Wahitimu walioko makazini kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa pamoja na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa maadili ikiwemo kujihusisha na vitendo vya Rushwa makazini.

 

 

 

UJUMBE KWA FACEBOOK