TTCL

Habari

Mavunde azindua mafunzo ya mafundi bidhaa za ngozi Mwanza  

on

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira,Watu wenye Ulemavu Antony Mavunde amezindua rasmi mpango wa mafunzo ya ufundi bidhaa za ngozi kwa njia za kisasa, kwa vijana 1000 wanaotaka mikoa zaidi ya kumi nchini.
Akizindua mpango huo leo hii Mjini Mwanza, Mavunde amesema mpango huo unalenga kujenga uwezo vijana kutengeneza na kuingiza sokoni bidhaa hizo.
Amezitaja baadhi ya bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo kuwa ni viatu, mikoba na mikanda,  ambazo soko lake bado ni kubwa nchini pamoja na nchi jirani.
Amesema, ujio wa mpango huo unaenda sambamba na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli inayohimiza Hapakazi tu, hivyo utasaidia kuwaandaa vijana kujiajiri na kuajiriwa kirahisi.
Aidha, amewataka vijana kutochagua kazi au kubweteka, kuwa kazi rasmi ni zile za ajira ya moja kwa moja serikali au sekta binafsi.
Amewataka vijana kubadili mtazamo wa maisha unaoendana na kusubiria ajira rasmi pekee, bali wafikirie zaidi kujiajiri.
Amesema mpango huu wa miaka mitano unalenga kuwafikia vijana zaidi ya milioni 4 nchini, ambao pia siyo tu utahamasisha vijana kujiajiri lakini pia utawaandaa vijana wengi kupata ujuzi utakaowaandaa kutumika katika mkakati wa kitaifa wa Taanzania ya viwanda.
Imetolewa na:
Idara ya Habari na Mawasiliano,
Wizara ya Kazi,Ajira,Ulemavu na Maendeleo ya vijana.

UJUMBE KWA FACEBOOK