TTCL

Habari

MBEYA KUTEKELEZA KWA VITENDO UCHUMI WA VIWANDA

on

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania ofisini kwake (hawapo pichani) kuhusiana na uchumi wa viwanda. Makamu Mwenyekiti wa TAJATI, Christopher Nyenyembe akimkabidhi zawadi ya Saa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla akipokea T Shirt la TAJATI kutoka kwa Makamu Mwenyekiti Nyenyembe Mtunza hazini wa TAJATI, Brandy Nelson akimkabidhi zawadi ya Saa ya ukutani Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja  huku Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wanachama wa TAJATI.

 

WAKURUGENZI wa Halmashauri za Wilaya zilizopo Mkoa wa Mbeya wametakiwa kuchagua mazao mawili kwa ajili ya kutafuta wawekezaji wa kuongeza thamani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais kuhusiana na uchumi wa viwanda.

Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipokuwa akizungumza na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) ofisini kwake kuhusu mikakati ya Mkoa katika kutekeleza azimio la Uchumi wa Viwanda.

Makalla alisema ametoa siku saba hadi ifikapo Juni 29, mwaka huu kila Halmashauri iwe imewasilisha ofisini kwake mpango kazi namna ya uanzishwaji wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao waliyoyachagua ambayo yanazalishwa kwa wingi katika maeneo yao.

Alisema katika kutekeleza adhma hiyo Mkoa umetoka na kauli mbiu isemayo “Mbeya ni lango la Uchumi na Utalii Nyanda za juu kusini” kutokana na sifa ambazo Mkoa unazo ambazo zinawezesha kuweza kuinuka kiuchumi na kuweza kupata mafanikiomakubwa.

Alizitaja sifa hizo kuwa ni kutokana na uwepo wa barabara kuu iendayo nchi za Kusini, uwepo wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, Historia ya kilimo cha maua na mazao ya mboga mbaoga na mradi mkubwa na Forodha katika mpaka wa Kasumulu kati ya Tanzania na Malawi sambamba na kukamilika kwa mradi mkubwa wa Meli za Mizigo katika Ziwa Nyasa.

Aliongeza kuwa katika Sekta ya Utalii Ukanda wa Nyanda za juu kusini unavyovivutio vikubwa na vya kipekee kuliko ukanda wa kaskazini lakini vimeshindwa kutangazwa na kuingizia mapato mikoa hiyo hivyo Mkoa umejikita katika kuhakikisha Utalii unakuwa sehemu ya vipaumbele vya Mkoa wa Mbeya.

Aidha alitoa wito kwa Waandishi wa habari hususani TAJATI kupigia kelele na kutangaza fursa za uwekezaji na Utalii katika Mkoa wa Mbeya ili uweze kuwa mfano namanufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja, aliwataka TAJATI kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili Mkoa uweze kupata manufaa kutokana na uwepo wa Chama chenye malengo sawa na Kauli mbiu ya Mkoa wa Mbeya.

Naye Makamu Mwenyekiti wa TAJATI, Christopher Nyenyembe alisema licha ya Chama hicho kuwa cha Kitaifa na makao makuu kuwa Mkoani Mbeya kipaumbele kikubwa ni kutangaza na kuibua masuala ya Utalii na Uwekezaji katika Mikoa ya Nyanda za Juu kusini.

 

 

 

UJUMBE KWA FACEBOOK