TTCL

Habari

RC MBEYA AHAMASISHA UTEKELEZAJI MRADI WA NHIF ‘TUMAINI LA MAMA’

on

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mbeya   kwenye ukumbi mdogo wa Mkapa jijini Mbeya

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya’ NHIF’  Bernard Konga akitoa taarifa ya uhamasishaji wa Mradi wa Tumaini la Mama kwa mkoa wa Mbeya    Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya (NHIF) Afya Kanda ya Mbeya, Issaya Shekifu akizungumza wakati wa kuhamisha mradi wa Tumaini la Mama ukumbi mdogo wa Mkapa Jijini Mbeya.

  Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudia Kitta akielezea mikakati ya wilaya ya Kyela kuupokea Mradi wa Tumaini la Mama

Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mgeni rasmi  Imani David Mratibu wa Mradi wa CHF na NHIF Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya na wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameziagiza Halmashauri za Mkoa wa Mbeya Kutelekeza Mradi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ‘Tumaini la Mama’ wenye lengo la kumkomboa Mwanamke kumpatia Huduma za Matibabu wakati wa Ujauzito.

Makalla amesema hayo wakati wa kikao cha Kazi cha kujadili Utekelezaji wa Mradi huo kwa viongozi na Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amesema kuwa kutokana na mradi huu kutofahamika vyema wakuu wa wilaya na watendaji wa Halmashauri za mkoa wa Mbeya wanatakiwa  kuutangaza ili ufahamike kwa wanajamii ikiwa ni pamoja na kusajili wananchi kwa lengo la kupatiwa kadi za Bima ya Afya.

Makalla amefafanua kuwa hadi sasa zaidi ya akina mama laki mbili wamekwisha patiwa huduma ya  Mama na Mtoto ambapo jumla ya kaya 248 kati ya kaya 408 zimefikiwa.

Amevitaka vituo kutumia fedha zilizotengwa ili kuboresha huduma chini ya usimamizi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ambao wanatakiwa kufuatilia na kufanya ukaguzi sanjari na kuhakikisha dawa zinafika kwa wakati katika zahanati na Vituo vya Afya.

Awali akizungumza wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika  katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya’ NHIF’  Bernard Konga amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu kwa mkoa wa Mbeya umeanza mwaka 2012.

Amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu kwa awamu ya kwanza ulihusisha mkoa wa Tanga na kwamba  katika awamu ya pili mradi huu umefika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Konga amesema kuwa sababu za mikoa hii kuwa ni ya kwanza katika mradi huu ulitokana na ongezeko la vifo vya Akina Mama na Watoto hadi kufikia mwaka 2012.

Aidha wakizungumza mpango mkakati wa utekelezaji wa Mradi huo Mkuu wa wilaya ya Chunya, Rehema Madusa na Mkuu wa wilaya ya Kyela Claudia Kitta wamesema kuwa wameupokea mradi huo kwa mikono miwili na kuwa umefika wakati unaostahili kutokana na changamoto zilizopo katika wilaya hizo.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK