TTCL

Habari

MILIONI 400 KUMALIZA TATIZO LA WENYE UALBINO NCHINI- MTAFITI

on

Mchungaji Andrew Mpora ambaye ni mtafiti wa virutubisho afya akionesha aina mpya ya mafuta kwa ajili ya matibabu ya ngozi kwa watu wenye Ualibino Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wenye Ualbino Mkoa wa Mbeya wakishuhudia utambulisho wa mafuta kwa ajili ya kutibu ngozi Baadhi ya Wageni wakishuhudia utambulisho wa mafuta kwa ajili ya kutibu ngozi Baadhi ya Mashuhuda na majirani wakifuatilia zoezi la kutambulisha mafuta ya kutibu ngozi yaliyogunduliwa na Mchungaji Andrew Mpora Baadhi ya Mafuta yaliyofanyiwa utafiti yakiwa bado hayajafungashiwa vizuri kutokana na kukosa usajili kutoka katika mamlaka husika.

 

ILI kukabiliana na changamoto ya Kansa ya ngozi inayowakumba watu wenye ualbino nchini, mmoja wa Watafiti wa Madawa na Tiba mkoani Mbeya amewaomba wadau na Serikali msaada wa fedha takribani Shilingi Milioni 400 ili aweze kutatua tatizo hilo.

 

Akizungumza wakati akitambulisha mafuta, Mtafiti huyo, Andrew Mpora alisema baada ya kusikia kilio cha Watu wenye Ualbino alianza kufanya utafiti kupitia vitabu mbalimbali na Semina katika Nchi za Kenya na Malawi tangu mwaka 2005 akitafuta tiba ya ngozi kwa ajili yao.

 

Alisema hivi karibuni amegundua dawa  ambayo ni virutubisho iliyotengenezwa kwa mchanganyiko wa alovera, Alizeti na ufuta ikiwa na uwezo wa kulainisha ngozi, kuzuia ngozi kutokana na miale ya jua ambayo ilikuwa ikipelekea ngozi za watu wenye Ualbino kuharibika.

 

Mpora alisema tayari ameifanyia majaribio kwa baadhi ya Watu wenye Ualbino na wasiokuwa nao kujaribu kutumia kwa muda wa Siku tatu hadi mwezi mmoja na kushuhudia kuwa ni nzuri na haina madhara kwa mwili wa binadam.

 

Alisema changamoto inayomkabili ni mlolongo wa kusajili na upatikanaji wa mashine kubwa ya kuweza kutengenezea mafuta tiba hayo pamoja na upatikanaji wa malighafi za kutosha ili aweze kusambaza nchi nzima na Nje ya Nchi jambo alilodai linahitaji shilingi Milioni 400 za Kitanzania.

 

Aidha alitoa Wito kwa Serikali kupunguza masharti ya usaji wa kiwanda na kuzipa usajili dawa hizo ili ziendelee kuwapunguzia maumivu wenye mahitaji kwani anatarajia kuanza kuziuza kwa Shilingi 5000 chupa moja tofauti na dawa wanazotumia kwa sasa ambazo zinauzwa bei ghali sana.

 

Kwa upande wake baadhi ya Waliotumia mafuta tiba hayo walisema ni mazuri kwa afya kwani licha ya kutibu na kuzuia ngozi kuharibika pia hutibu magonjwa mengi mwili ikiwemo Pumu, miguu kuwaka moto, Presha ya kupanda na kushuka pamoja na uchovu wa mwili.

 

Claud Mwakyoma ni Mwenyekiti wa Watu wenye Ualbino Mkoa wa Mbeya alisema ni vema Serikali kupitia TBS, TFDA na SIDO kupitia haraka mafuta hayo ili kujua madhara ya binadamu kama yapo ili iweze kuboreshwa kabla ya kuingizwa sokoni kutokana na kuonekana ni mkombozi kwao.

 

Alisema Mkoa wa Mbeya pekee una Watu wenye Ualbino zaidi ya 200 ambao asilimia kubwa wanakabiliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi kutokana na kushindwa kumudu gharama za kununulia mafuta ambayo huuzwa kati ya shilingi 25,000 hadi 45000 hivyo kupatikana na mafuta mbadala kutaokoa maisha ya wengi.

 

Naye William Simwali Katibu wa Wenye Ualbino Wilaya ya Mbeya alisema alikuwa mtu wa kwanza kupewa mafuta hayo na kuanza kuyatumia baada ya siku tatu aliona matokeo mazuri ndipo alipowapa na wenzie kuyajaribu na wao kwa pamoja kukubaliana kuwa mafuta hayo ni mkombozi wao.

 

Alisema ni vema Serikali kupitia mashirika na Mamlaka mbalimbali ikamsaidia mtafiti huyo kumuwezesha kupata usajili, vifungashio na uwezo wa kuzalisha kwa wingi ikiwa pia ni mtekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchumi wa viwanda.

UJUMBE KWA FACEBOOK