TTCL

Habari

MILIONI 60 ZAHITAJIKA KUJENGA KANISA

on

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Omega Groly Ministry, Joshua Mwaijengo akiendesha ibada kabla ya kuanza kwa Harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo. Mgeni rasmi katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Omega, Michael Nyilawila akitoa ahadi ya fedha kwa ajili ya kuchangia wakati wa harambee Nambwike Lazaro akisoma risala ya kanisa kwa mgeni rasmi Waumini wa Kanisa la Omega wakiwa kwenye kanisa ambalo limezungushiwa maturubai

ZAIDI ya shilingi milioni 60 zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la Omega Glory ministry for all nation lililopo Sae jijini Mbeya ambapo hivi sasa waumini wa Kanisa hilo wanaabudia kwenye hema lililozungushiwa maturubai.

Akizungumza katika harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo, Mchungaji kiongozi,Joshua Mwaijengo alisema Kanisa limepata kiwanja kwa ajili ya ujenzi kinachohitajika na fedha na vifaa kutoka kwa wadau na waumini.

Alisema baada ya kuona nguvu za waumini katika kuchangishana imekuwa ndogo kutokana na kutofautiana kwa vipato wakaona ni vema kushirikisha wadau wengine kupitia harambee hiyo.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi, mjumbe wa kamati ya ujenzi, Nambwike Lazaro alisema katika kufikia malengo ya ujenzi waumini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa fedha ingawa tayari wamefanikiwa kupata kiwanja eneo la Uyole.

Alisema matarajio ya waumini ni kuanza ujenzi wa kanisa hilo mapema mwaka huu kwa thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 60 ambapo fedha hizo wanategemea kuzipata kutoka kwa waumini na wadau wa maendeleo bila kujali imani zao.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika Harambee hiyo, Michael Nyilawila maarufu kwa jina la mzee wa masauti ambaye pia ni mshehereshaji maarufu mkoani Mbeya aliwaungoza waumini wa kanisa hilo kukusanya shilingi Milioni 15.

Nyilawila akizungumza katika harambee hiyo alitoa wito kwa waumini na wadau mbalimbali kujitolea kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.

Alisema yupo tayari kuendelea kushawishi marafiki mbali mbali kujitokeza kuchangia ujenzi huo ili uanze mara moja baada ya fedha kupatikana.

“Ujenzi wa kanisa utafanikishwa na sisi wenyewe ila niwaahidi kuwa siku moja nitawashawishi marafiki zangu tuje tuabudie hapa na kuchangishana ili kufanikisha ujenzi wa kanisa hili”alisema Nyilawila.

UJUMBE KWA FACEBOOK