TTCL

Makala

MJUE SAMAKI ANAYEONGOZA KWA UTAMU ZIWA NYASA

on

Anaitwa Likuku ambaye ni jamii ya samaki aina  ya perege mkubwa.Wavuvi wanamtaja samaki huyo kuwa ana kichwa chenye kipara,rangi angavu.Ndiye samaki anayependwa kuliwa na ndege aina ya Ngwazi(eagle) ambaye anapatikana ziwa Nyasa.Ndege huyu ana sifa ya kula vitu flesh.Kutokana na utamu wa samaki huyo Ngwazi inamlazimu kukaa angani umbali wa mita 120  kwa saa sita bila kutua hadi anapofanikiwa kumuona samaki huyo, hushuka kwa kasi na kumkata.Hata hivyo samaki huyo yupo katika hatari ya kutoweka katika ziwa Nyasa kutokana na uchafuzi wa maji katika ziwa hilo.Kwa mujibu wa utafiti wa SADC ambao ulifanyika katika ziwa Nyasa  kati ya mwaka 1991 hadi 1994 na mwaka 1996 hadi 2000,ziwa Nyasa lina kiasi cha tani 165,000 za samaki wa aina mbalimbali.
Na Albano Midelo

UJUMBE KWA FACEBOOK