TTCL

Habari

Mkuu wa Wilaya ya Chunya awapa wiki moja wafanyabiashara ya mafuta kufunga mashine za EFDs.

on

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Rehema Madusa 
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Rehema Madusa amewataka wafanyabiashara wa vituo vya mafuta ya magari na mitambo kufunga mashine za EFDs kuanzia Septemba 8 mwaka huu. Ameyasema hayo katika semina iliyojumuisha mamlaka ya mapato Wilaya ya Chunya(TRA)na wafanyabiashara baada ya kubaini vituo vyote kutokuwa na mashine za EFDS  hivyo kuikosesha serikali mapato.Aidha Madusa amesema kuwa wananchi wengi hawana kawaida ya kudai risiti hivyo wafanyabiashara hao kuitumia nafasi hiyo kuwadhulumu wananchi na kuikosesha kodi inayotokana na mauzo ya mafuta.Amewaagiza maafisa wa TRA kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuwabaini wafanyabiashara watakaokaidi agizo hilo. Mkuu wa Wilaya amesema kuwa ufungwaji wa mashine za EFDs utaongeza mapato ya serikali ili kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli kuwataka wafanyabiashara  kulipa kodi na wananchi kudai risiti ili serikali iweze kujitegemea na kuwaletea maendeleo kwa kutoa huduma bora kwa raia kama elimu, maji, umeme, barabara, afya nk.Baadhi ya wafanyabiashara wa vituo vya mafuta waliohudhuria semina hiyo ni kutoka Chunya mjini, Matundasi na Makongolosi.

UJUMBE KWA FACEBOOK