TTCL

Habari

MSHEIKH MBEYA WAWAFUNDA WANAZUONI VYUO VIKUU.

on

*Ni katika mahafali ya wanaohitimu VYUO vikuu  kwa Jumuiya ya TAMSYA.

ELIMU NA MALI

Na Sheikh Dourmohamed Issa
“Fadhila za Elimu ni kubwa,Elimu ni tofauti na mali,Elimu inaongezeka kadri unavyoitumia na Mali hupungua kadri unavyoitumia.

” Elimu mliyoipata isiwajengee Kiburi,mkawadharau hata mama zenu na wazazi wenu, Pepo iko chini ya miguu ya Mama zenu,
Vitu viwili vinaenda pamoja, Tabia Njema na Elimu, nendeni mkawe waadilifu mkiwa makazini.

UJASIRIAMALI
Na Sheikh KHALFAN El Riyami
Tujitahidi kuwa na fikra chanya katika kufikia malengo Yetu, na ukiamua kufanya biashara unapaswa kuipenda na kuithamini ili ikupe mafanikio.

NDOA
Na Sheikh Bombo Ibrahim
Msiogope kutafutiwa wachumba wa kuwaoa au kuoa,kwani lengo la ndoa ni muunganiko wa wawili mke na mume wenye nia ya Kupata Starehe na utulivu wa nafsi na kutengeneza kizazi CHEMA.
KUTEMBEA UCHI SIO USOMI

Na Dr Suley Hassan
Mavazi ya stara yanaleta heshima,kutembea UCHI sio usomi wala si mila na desturi za kiislamu,muendako mkautangaze uislamu na desturi zake na mjifakharishe nao  uislamu wenu.

Na Rashid Mkwinda

UJUMBE KWA FACEBOOK