TTCL

Habari

MWENGE WAZINDUA MIRADI YA SHILINGI BILIONI 1.6 JIJINI MBEYA

on

Mwenge wa Uhuru 2018 ukiwaka katika uzinduzi wa  moja ya miradi  jijini Mbeya.Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Charles Kabeho akiweka Jiwe la Msingi katika moja ya Miradi ambayo ilizinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2018.

MWENGE wa Uhuru 2018 umezindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi sita yenye thamani ya shilingi 1,610,621,915 katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

 

Miradi hiyo ni pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi katika  ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi Azimio yanayojengwa kwa fedha kutoka serikali kuu shilingi 139,649,885.

 

Mradi mwingine ni ufunguzi wa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi katika kituo cha afya Kiwanjampaka wenye thamani ya shilingi 42,361,030.

 

Mwenge huo pia ulizindua mradi wa Maji Iziwa (374,892,000),Kiwanda cha Banana wine kilichopo Kalobe (150,000,000), ujenzi wa kituo cha malezi na makuzi ya watoto Itanji kata ya Iganjo(72,141,000).

 

Mwenge pia aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Lami ya Isyesye hadi Itezi  yenye urefu wa kilomita mbili kwa thamani ya shilingi 831,578,000.

 

Wakati huo huo Kiongozi  wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2018, Charles Kabeho amewataka Watendaji nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi inatekelezwa kutokana na fedha za Serikali.

 

Kiongozi huyo alitoa wito huo juzi wakati Mwenge wa Uhuru ulipokuwa ukikimbizwa katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambapo miradi sita iliwekewa mawe ya msingi, kufunguliwa sambamba na kuzinduliwa.

 

Alisema Wataalam wanashindwa kusimamia vizuri miradi hali inayopelekea kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha za umma kwa baadhi ya miradi kujengwa chini ya viwango huku fedha nyingi zikiwa zimetumika.

 

Mbali na usimamizi pia aliagiza wakandarasi wanaopewa dhamana ya utekelezaji wa miradi kumaliza kazi hizo kwa wakati unaokusudiwa ili kutimiza malengo na makubaliano ya kimkataba.

 

 

 

 

UJUMBE KWA FACEBOOK