TTCL

Habari

NOAH YAUA WATU 8 MBEYA.

on

Gari aina ya Noah likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la abiria huku watu nane waliokuwa kwenye Noah wakipoteza maisha na mmoja kujeruhiwa Vikosi vya uokoaji vya Jeshi la Polisi na Zimamoto Mbeya wakiondoa miili ya marehemu kwenye gari aina ya Noah Wakazi wa Jiji la Mbeya wakishangaa ajali ya Gari iliyoondoa maisha ya watu nane waliokuwa wakisafiri na Noah kutoka Chunya kwenda Mbeya Basi lililosababisha ajali ya Noah likiwa limeharibika kidogo  sehemu ya Mbele ya Basi hilo lililokuwa likienda Chunya kutoka jijini Mbeya Wakazi wa Jiji la Mbeya wakishuhudia uokoaji wa majeruhi wa ajali ya Noah iliyogongana na basi eneo la Mwansekwa

 

WATU nane wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi kubwa la abiria na gari dogo aina ya Noah.

 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba imetokea leo Aprili 9, mwaka huu katika eneo la Maili tano Kata ya Mwansekwa barabara ya Chunya Mbeya.

 

Alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa tano asubuhi ambapo gari dogo aina ya Noah lenye namba za usajili T 649 DEA likiwa na abiria tisa likitokea Chunya kuelekea Mbeya liligongana uso kwa uso na Basi la abiria lenye namba T 672 CLR lenye jina la Igembe Nsabo likitokea Mbeya kuelekea Chunya.

 

Alisema Gari dogo lilikuwa likiendeshwa na Juma Lihinda huku gari kubwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina moja la Abdalah ambaye alikimbia mara baada ya ajali hiyo.

 

Kaimu Kamanda alisema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye akiwa anapanda mlima alihama kwenye upande wake na kuhamia upande mwingine ambapo gari dogo likiwa mwendokasi likaingia kwenye basi.

 

Aliwataja marehemu kuwa ni wanaume watatu na wanawake watano ambao walitambuliwa kwa majina kuwa ni Dereva wa Noah Juma Lihinda, Alphatel Mihava (mkosa sura),Husna Lusambo na  Jackline Charles wote wakazi wa Chunya.

 

Alisema majeruhi amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya anakoendelea na matibabu na kwamba Dereva wa basi natafutwa na jeshi la Polisi ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK