TTCL

Michezo

Pogba uwenda akaikosa Manchester Derby

on

Kocha wa Manchester United amepata hofu kuwa Paul Pogba anaweza kuikosa mechi ya Alhamisi dhidi ya Manchester City maarufu kama Manchester Derby baada ya kupata majeraha dhidi ya Burnley wikiendi iliyopita.

Mourinho alisema kuwa hajui kama Pogba aliumia au alikuwa amechoka, lakini kocha huyo wa Mashetani Wekundu amesema kuna uwezekano mkubwa nyota huyo akaikosa mechi ya Alhamisi katika uwanja wa Etihad.

Sijui kama ameumia au ni uchovu wa misuli tu, sijui kwa kweli. Lakini kama hataweza kucheza Alhamisi, basi hatacheza. Tutachezesha mchezaji mwingine na hatuna sababu ya kulia,” Mourinho, ambaye tayari amewakosa Chris Smalling, Phil Jones, Marcos Rojo, Juan Mata na Zlatan Ibrahimovic, aliwaambia waandishi.

UJUMBE KWA FACEBOOK