TTCL

Habari

POLISI MBEYA YAKUSANYA BILIONI 2 KWA MAKOSA BARABARANI 2017.

on

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika katika Stendi ya mabasi Nanenane. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga akielezea jinsi Jeshi la Polisi lilivyojipanga katika kuzuia ajali  katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika katika Stendi ya mabasi Nanenane. Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Mbeya, Allan Mwaigaga akielezea umuhimu  wa elimu kwa watumiaji wa barabara katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika katika Stendi ya mabasi Nanenane. Katibu wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya, Leopard Fungu akisoma risala  katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika katika Stendi ya mabasi Nanenane. Chifu wa Mkoa wa Mbeya, Roketi Mwashinga akizungumza jambo katika maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama barabarani  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akipata maelezo kutoka kikosi cha zimamoto na uokoaji  katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika katika Stendi ya mabasi Nanenane. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akisikiliza wadau wa usalama barabarani  katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika katika Stendi ya mabasi Nanenane. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akipata maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya simu ya TTCL  katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika katika Stendi ya mabasi Nanenane. Askari wa Jeshi la uokojai na zimamoto wakionesha namna ya kuzima moto kwa kutumia kifaa maalum Mdau wa usafirishaji akipita mbele ya maandamano na gari analotumia kufundishia wanafunzi wa udereva Askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha ukaguzi wa magari wakionesha namna wanavyofanya ukaguzi wa gari kabla halijaruhusiwa kuanza safari Baadhi ya wananchi na madereva wakiwa wamejitokeza katika sherehe za wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoani Mbeya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya askari wa Kikosi cha usalama barabarani wakati wa  kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika katika Stendi ya mabasi Nanenane.

 

JESHI la Polisi kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kupunguza ajali kwa asilimia 38   kutoka ajali  393 mwaka 2016 hadi kufikia ajali 244 mwaka 2017.

 

Aidha Jeshi hilo pia limefanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni mbili kutokana na tozo za makosa ya usalama barabarani kwa mwaka 2017 ikiwa ni ongezeko la Shilingi Milioni 459 kwa mwaka 2016.

 

Hayo yalibainishwa wakati wa Sherehe za kilele cha maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama barabarani Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika Stendi ya mabasi ya nanenane jijini Mbeya.

 

Akisoma risala ya Maadhimisho hayo, Katibu wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya, Leopard Fungu ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya (RTO) alisema idadi ya ajali iliyopungua ni 149.

 

Alisema Mwaka 2016 kulikuwa na Jumla ya ajali 393 kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Disemba  ambapo jumla ya ajali za vifo zilikuwa 182, idadi ya waliofariki 205,ajali za majeruhi 211 na idadi ya majeruhi ikiwa ni 479.

 

Alisema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Disemba 2017 jumla ya ajali ni 244 huku ajali za vifo zikiwa 141, idadi ya waliofariki 170, ajali za majeruhi 98 na waliojeruhiwa wakiwa 268 hivyo kuwa na punguzo la asilimia 38.

 

Alisema kuhusu tozo katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Disemba 2016 jumla ya makosa yalikuwa 65779 na makosa yaliyolipa tozoyalikuwa 64030 na kupelekea kukusanya fedha shilingi 1,920,900,000/=.

 

Aliongeza kuwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2017 jumla ya makosa yalikuwa 81967 na yaliyolipa tozo yalikuwa 79335 yaliyoingiza shilingi 2,380,050,000/=.

 

Kamanda huyo alisema jumla ya makosa yaliyoongezeka kwa kiindi cha 2016 hadi 2017 ni 16188 ambapo yaliyolipa tozo ni makosa 15305 na kuingiza shilingi 459,150,000/=.

 

Alisema sababu ya kuongezeka kwa makosa hayo ni kutokana na kuwepo kwa vifaa vya kupima mwendokasi wa magari ambapo Askari hufanya kazi kwa kificho nakuhamahama.

 

Alisema ili kupunguza ajali na makosa barabarani Jeshi limejipanga kutoa elimu katika Shule za Msingi na Sekondari kuhusu alama na michoro ya barabarani.

 

Kwa upande wake Mgeni rasmi wa sherehe hizo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alitoa wito kwa Jeshi la Polisi kuendelea kudhibiti madereva wa bodaboda na Bajaji ili wawe na leseni za kuendeshea vyombo vyao.

 

Makalla pia alitoa Rai kwa Jeshi la Polisi kuacha vitendo vya kupokea Rushwa barabarani kwamba kitengo hicho kinaharibu picha na uaminifu wa Jeshi kwa wananchi.

 

Aidha aliagiza Jeshi hilo kutilia mkazo wa ukaguzi wa magari kabla ya kuanza safari ili kupunguza ajali pamoja na abiria kuacha kutupa taka hovyo na badala yake kila gari linapaswa kuwa na chombo cha kutunzia taka.

 

Mkuu wa Mkoa pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya mkoani Mbeya kufanya operesheni maalum ya kuwaondoa wafanyabiashara waliopanga pembezoni mwa barabara kwa kuwa wanahatarisha maisha yao.

 

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Mbeya, Allan Mwaigaga alisema mafanikio ya kupunguza ajali mkoani Mbeya yametokana na elimu kwa madereva sambamba na utii wa sheria bila shuruti.

 

Alisema lengo ni kuhakikisha ajali zinaisha kabisa katika Mkoa kwa kuendana na kauli mbiu ya maadhimisho hayo inayosema zuia ajali, tii sheria, okoa maisha.

UJUMBE KWA FACEBOOK