TTCL

Habari

PROFESA LUHANGA AWAASA WAHITIMU MZUMBE KAMPASI YA MBEYA

on

Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Jaji mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta akiwatunuku Wahitimu wa Mzumbe Kampasi ya Mbeya Astashahada, Stashahada na Shahada mbalimbali katika Mafahali ya 16 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Chuo kikuu Mzumbe, Profesa Matthew Luhanga akihutubia katika sherehe za Mahafali ya 16 ya Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka akiwahutubia Wahitimu wakati wa Mahafali ya 16 ya Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Naibu Makamu Mkuu wa  Chuo taaluma Prof Ganka Nyamsogoro akiwahudhurisha wahitimu wa fani mbalimbali kwa ajili ya kutunukiwa na Mkuu wa Chuo wakati wa Mahafali ya 16 ya Kampasi ya MbeyaBaadhi ya Viongozi waandamizi wa Chuo kikuu Mzumbe na wageni mbalimbali wakiwa jukwaa kuu wakati wa mahafali ya 16 ya Chuo cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Baadhi ya Watumishi na Wakufunzi wa Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya wakifuatilia sherehe za Mahafali ya 16 ya Mzumbe yaliyofanyika katika Kampasi ya Mbeya iliyopo Forest ya zamani jijini Mbeya Baadhi ya Wahitimu wakiwa na nyuso za furaha wakati wa sherehe za Mahafali ya 16 ya Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Baadhi ya Wazazi na Wageni waalikwa wakifuatilia sherehe za mahafali ya Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Wakufunzi wa Chuo kikuu Mzumbe wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye sherehe za Mahafali ya Chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Mbeya. Brass band ya Jeshi la Magereza ikiongoza maandamano kuelekea katika viwanja vya sherehe kwa ajili ya Mahafali ya Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya.

 

MWENYEKITI wa Baraza la Ushauri la Chuo kikuu Mzumbe, Profesa Matthew Luhanga amewataka wahitimu wa fani mbalimbali katika chuo hicho kuwa chachu na mfano wa kuigwa kwenye jamii.

 

Profesa Luhanga alitoa wito huo jana wakati wa Mahafali ya 16 ya Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya ambapo alisema Wahitimu baada ya kutunukiwa Astashahada, Stashahada na Shahada zao wanakuwa miongoni mwa nguvu kazi kwa ajili ya kuleta chachu ya maendeleo katika jamii.

 

Alisema wanapaswa kutumia ujuzi na elimu waliyoipata kutatua changamoto mbalimbali katika jamii ikiwemo kujiajiri wenyewe ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya kuelekea kwenye uchumi wa Viwanda.

 

Aidha alitoa wito pia kwa wahitimu hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi kuepuka kujipatia kipato kinyume na taratibu ambacho sio halali, kujiepusha na vitendo vya Rushwa na ufisadi.

 

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka alisema jamii ya wakazi wa Nyanda za juu kusini na Nchi jirani wamekipokea vizuri Chuo Kampasi ya Mbeya na kukipatia mafanikio.

 

Alisema tangu Kampasi ya Mbeya ianzishwe mwaka 2006 ilikuwa na wahitimu 405 wakiwa na program 2 lakini waliohitimu mwaka huu ni 734 katika program 11.

 

Alisema kutokana na mwitikio huo matarajio ni kudahili wanafunzi 900 baada ya kukamilisha kutatua changamoto ya miundombinu ikiwemo madarasa na kumbi za mihadhara.

 

Aidha aliupongeza uongozi wa Mkoa wa Mbeya sambamba na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kuukubalia uongozi wa Chuo na kuwapatia eneo lililopo Iwambi kwa ajili ya ujenzi wa Chuo.

 

Alisema ujenzi wa Chuo eneo la Iwambi utaenda hatua kwa hatua na litaendelezwa kwa viwango vya hali ya juu ili Chuo kikuu Mzumbe kiwe mfano wa vyuo vingine ndani na nje ya Nchi.

 

Hata hivyo alitoa wito kwa jamii, wadau na wawekezaji kujitokeza katika kuendeleza na kuwekeza kwenye miradi katika eneo la Iwambi ikiwemo ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi na vitega uchumi mwingine.

 

Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Jaji Mstaafu, Barnabas Samatta aliwatunuku Astashahada, Stashahada na Shahada wahitimu 734 wakiwemo wanawake asilimia 50.1 na wanaume asilimia 49.9 katika fani mbalimbali ikiwemo Sheria, Biashara na manunuzi.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK