TTCL

Habari

SHULE BINAFSI ZAONYWA

on

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu akitoa hotuba ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto Afrika yaliyofanyika kimkoa katika Jiji la Mbeya ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Mkurugenzi wa Shirika la Child Support Tanzania, Noela Shawa akielezea namna shirika hilo lilivyosaidia Watoto wengi wenye mahitaji maalumu kujiunga na shule za awali na Msingi mkoani Mbeya Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya, Stella Kategile akifafanua jambo katika sherehe za Siku ya Mtoto Afrika zilizofanyika Kimkoa jijini Mbeya Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Child Support Tanzania, Julius Kaijage akitoautambulisho kwa wageni mbalimbaliwaliohudhuria maadhimisho ya siku ya mtoto Afrikamkoani Mbeya. Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Jeremiah Minja akielezea namna Mkoa wa Mbeya ulivyotekeleza mahitaji ya watoto katika sherehe za Mtoto Afrika. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu akiangalia bidhaa mbali mbali zinazotengenezwa na vijana wajasiliamali mkoani Mbeya. Watoto wa Shule za Msingi jijini Mbeya wakitumbuiza katika Siku ya Mtoto Afrika mkoani Mbeya. Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho ya siku ya Mtoto Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi.

 

SERIKALI imezipiga marufuku Shule za Sekondari za binafsi na mashirika yasiyokuwa ya umma kupanga wastani mkubwa wa ufaulu kwa wanafunzi kutoka kidato kimoja kwenda kingine kisha kuwafukuza wasiofikisha alama hizo.

Marufuku hiyo imepigwa na Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na Sayansi ya Teknolojia, Dk. Ave Maria Semakafu alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari mara baada ya kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika yaliyoadhimishwa katika Mkoa wa Mbeya ambapo alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stellah Manyanya.

Alisema hivi sasa shule za umma zinaonekana hazina ufaulu ukilinganisha na shule za watu binafsi jambo ambalo sio la kweli kwani Serikali inahakikisha kila mwanafunzi anapelekwa shule ili apate Elimu lakini Wamiliki wa shule Binafsi wanachopigania ni kuongoza kwenye ufaulu kwa kubagua watoto wenye ufaulu mzuri.

Alisema kuanzia sasa hakuna Mwalimu wala Shule kumtimua mwanafunzi shule ambaye hakufikisha wastani ambao upo kwa mujibu wa utaratibu wa Wizara na Sera ya Elimu tofauti na wastani mkubwa unaopangwa na shule ambao huwabauga baadhi ya watoto na wao kuchukua wenye uelewa pekee.

“Nashangaa unajiita shule nzuri inayofaulisha vizuri lakini kumbe kazi yako ni kuengua wenye uwezo pekee na hao wengine unamwachia nani la sivyo tuelewe kuwa shule yako haina Walimu wa kuweza kuwafundisha wanafunzi wasio na uwezo binafsi, Hivyo kuanzia sasa marufuku mtoto kufukuzwa kwa kushindwa kufikisha wastani wa 61 mliojipangia” aliagiza Naibu Katibu mkuu.

Aliongeza kuwa shule itakayobainika kuendelea kuwafukuza watoto kutokana na kutofikisha Wastani mkubwa    Serikali haitasita kuwachukulia hatua wahusika vinginevyo wafuate utaratibu wa uliowekwa na Wizara ikiwa ni pamoja na kuendesha shule kwa ushindani wa kumsaidia mzazi na mwanafunzi.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya watoto wa Mkoa wa Mbeya,Feith Johnson alisema ni vema Serikali ikawekeza kwa kutoa elimu kwa watoto bila ubaguzi ikiwemo kusimamia elimu jumuishi ambayo itaondoa ubaguzi kati ya Wenye ulemavu na wasio na ulemavu.

 

 

UJUMBE KWA FACEBOOK