TTCL

Habari

Taarifa ya watoto walioko Marekani kwa matibabu

on

UPDATE:

HIVI PUNDE, Mercy Hospital, Sioux City IA:

MTOTO Sadia akiwa na Dkt. Steve Joyce, ambaye ni Daktari wake wa “Internal Medicine”. MADAKTARI wanasema Binti Sadia ni MUUJIZA wa Mungu kutokana na HALI aliyokuwa nayo KABLA ya huduma ya UPASUAJI. Asanteni SANA kwa DUA na SALA zenu

UPDATE:

Mei 18, Alhamisi

MTOTO Wilson kwa mara KWANZA ametoka NJE ya Jengo Kuu la Hospital ya Mercy akiwa kwenye “wheelchair”, huku Mama na Daktari wake wakiwa na TABASAMU***

Latest UPDATE:

Mei 18, Alhamisi

Saa 4:30 Usiku (Masaa ya Afrika Mashariki)
Habari za HIVI PUNDE kutoka Hospitali ya Mercy, Sioux City IA
MTOTO Doreen amemaliza KUFANYIWA UPASUAJI wa UTI wa MGONGO, kwa KILE ambacho MADKTARI wamesema kumefanikiwa kwa UFANISI Mkubwa, KUPITA matarajio yao. MTOTO Doreen alikuwa afanyiwe UPASUAJI kwa makadrio ya MASAA 5:30, LAKINI zoezi HILO lilikamilika kwa muda wa MASAA 4:00, Huku TEAM ya “Surgical Support” IKIWA na watu 6, na kwa PAMOJA wakiongozwa na MADAKTARI BINGWA 2, Dr. Meyer na Dr. Durward. MTOTO Doreen amehamishwa KUTOKA chumba cha UPASUAJI na kupekewa ICU, na MADAKTARI wamesema KWAKUWA hali yake imeridhisha SANA, BAADAYE Leo watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya UPASUAJI, na kumrudisha WODI ya WATOTO ambako ataendelea na MAPUMZIKO. MUNGU amesikia

MAOMBI ya WATANZANIA na WOTE waliotoa SALA na DUA zao kwa ajili ya MTOTO Doreen POPOTE Duniani.

Na Lazaro Nyarandu

UJUMBE KWA FACEBOOK