TTCL

Habari

TAWA YAFADHIRI MAFUNZO KWA WANAVIJIJI WAPATAO 25 KUTOKA TUNDURU

on

                             Mhe.Luckiness A. Amlima(Mkuu wa wilaya ya Namtumbo) akiongea na wahitimu

 

Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) imefadhiri mafunzo kwa wanavijiji wapatao 25 kutoka    Wilaya ya Tunduru wenye kero za wanyamapori wakali na waharibifu hususani mnyama Tembo

Wahitimu wanajiji 25toka Tunduru wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Namtumbo(Aonekani kwenye picha hii)

Wahitimu walijifunza mbinu mbalimbali Za kumthibiti Tembo kuingia shambani na kula mazao
Njia walizojifunza ni pamoja na kutumia Pilipili iliyochanganywa na kinyesi cha Tembo na kuzungusha shambani kwa kuchoma moshi wenye pilipili Tembo wanakimbia.

Kinyesi cha  Tembo kimeshawekwa pilipili

Mkuu wa chuo akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi

Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu-TAWA Bw. Munuo alitoa hotuba yake kwa kusema. TAWA itaendelea kusimamia morogoro baina ya wanyamapori na wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali

Mkuu wa wilaya akipata maelezo ya vitamba vyenye oil chafu toka kwa mhitimu

Njia nyingine waliyojifunza ni kutumia mizinga ya nyuki kuzungushia shsmba na kufunga wire Tembo akigusa wire mizinga inajitingisha na nyuki kutoka na kulia Tembo anakimbia angalia picha zinazofuata

 

Taarifa hii imetolewa na Bw. Twaha Twaibu (Afisa Habari -TAWA)

 

 

UJUMBE KWA FACEBOOK