TTCL

Habari

TCRA YAKABIDHI RASMI LESENI KWA MTANDAO WA MBEYA YETU.

on

Mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa mbeyayetu, Joseph Mwaisango (kushoto) akiwa na John Bukuku mmiliki wa Blog ya Full Shangwe wakionesha Leseni  za uendeshaji wa mitandao ya kijamii baada ya kukabidhiwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa mbeyayetu, Joseph Mwaisango (kushoto) akiwa na John Bukuku mmiliki wa Blog ya Full Shangwe wakifurahi mbele ya jengo la  Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Leseni ikionesha kibali kwa Mtandao wa mbeya yetu kufanya kazi za kihabari kihalali kwa mujibu wa Sheria

Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa MBEYA YETU MULTIMEDIA COMPANY inayomiliki Mtandao wa Mbeya Yetu Online Tv,Mbeya Yetu Website na Mbeya Yetu Magazine inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuthamini mchango wa Blogers nchini.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia TCRA imethamini na kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari na kuwatambua rasmi Mabloger kama ni sehemu inayopaswa kurasimishwa na kupewa usajili  na kuwa vyombo kamili vya habari.

Tulisubiri fursa hii kwa muda mrefu na sasa tunaanza kuona nyota inayoangaza kwa kupewa fursa ya kufanya kazi kwa utaratibu, kanuni na sheria zinazotambulika rasmi kama mhimili wa nne usiorasmi.

Tunatumia fursa hii kuwashukuru Blogers wote nchini ambao kwa namna moja ama nyingine tumekuwa tukishirikiana katika kupeana taarifa znazohusu tasna yetu ya habari.

Shukrani za dhati ziende kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Mbeya ambayo kwa namna moja ama nyingine imechangia kutoa hamasa na hata kututambua kazi zetu sanjari na kutusisitiza tufanye kazi kwa kuzingatia maadili.

Aidha tunatumia fursa hii kuwashukuru wadau wa habari waandishi wa habari wa mikoa ya Mbeya, Iringa,Njombe, Ruvuma,Rukwa, Katavi na Songwe kwa ushauri wenu wa mara kwa mara kwetu hata tumefikia hatua hii kuwa ni Mtandao wa Kwanza wa Online kupata leseni kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Hatutasita kutoa shukrani zetu kwa viongozi wote wa serikali na vyama vya siasa ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakithamini mchango wetu katika jamii na hata kututumia katika kuihabarisha jamii.

Tunatoa wito kwa Wanahabari wenzetu kushirikiana na kujenga upendo na mshikamano tukiamini katika ushirikiano na upendo ndipo tunapoweza kusimama imara na kupiga hatua katika kuijenga Mbeya Yetu na maendeleo yetu binafsi.

Mbeya Yetu Online Tv pamoja na mtandao wa Full Shangwe unayomilikiwa na Bloger John Bukuku vimekuwa ni vyombo vya kipekee kuchukua leseni leo hii Juni 6,2018 baada ya kundi la kwanza la vyombo vikubwa vya habari nchini pamoja na  Mitandao 45 kupata Leseni Mei 25 mwaka huu.

UJUMBE KWA FACEBOOK