TTCL

Habari

TTB, WATANZANIA TEMBELEENI VIVUTIO VYA NDANI

on

Afisa uhusiano mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Geofrey Tengeneza akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya kuhamasisha watanzania kutembelea vivutio vya utalii vya ndani. Afisa uhusiano mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Geofrey Tengeneza akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni ya kuhamasisha watanzania kutembelea vivutio vya utalii vya ndani. Baadhi ya Waandishi wa habari mkoani Mbeya wakimsikiliza Afisa Uhusiano wa Bodi ya Utalii (haupo pichani) kuhusu kampeni ya kuhamasisha Watanzania kutembelea vivutio vya ndani vya utalii.

 

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imetoa wito kwa watanzania kupenda kutembelea vivutio vya utalii vya ndani kwa lengo la kukuza na kuinua pato la Taifa.

Wito huo ulitolewa jana na Afisa uhusiano mkuu wa Bodi ya Utalii, Geofrey Tengeneza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya kuhusiana na Kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani iliyozinduliwa mkoani Mbeya.

Tengeneza alisema Bodi ya Utalii ilifanya utafiti mwaka 2006 na kubaini kuwa idadi kubwa ya Watanzania hawatembelei vivutio vya Utalii vya ndani na badala yake wanajua kazi ya Utalii ni ya wageni kutoka nje ya Nchi.

Alisema baada ya kugundua uwepo wa changamoto hiyo Bodi ilianzisha kampeni mbali mbali za kuhamasisha utalii wa ndani mwaka 2007 ambapo idadi ilianza kuongezeka kutoka watalii 250,000 hadi zaidi ya 800,000 sasa.

Alisema matarajio ya Bodi ni kuona utalii wa ndani unaingiza pato kubwa kwa Taifa bila kutegemea Utalii wa Kimataifa hivyo kuendelea kuendesha kampeni zingine zaidi.

Alisema kutokana na kuonekana Wananchi bado wanahitaji elimu zaidi kuhamasishwa kutembelea vivutio vya utalii vya ndani Mei 3, mwaka huu Bodi ilizindua kampeni mpya.

Aliitaja kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa katika Mkoa wa Kigoma na kuendelea katika mikoa minne kuwa ni “Utalii wa ndani uanze na mtanzania mwenyewe”.

Aliongeza kuwa baada ya kuzindua kampeni hiyo mkoani Kigoma Bodi ilizindua tena katika Mkoa wa Iringa na sasa Mbeya kisha Mkoa wa Mwanza.

Akizungumzia uzinduzi wa kampeni hiyo katika Mkoa wa Mbeya alisema itafanyika katika viwanja vya Uhasibu kuanzia majira ya saa moja jioni ambapo Agape Television Network(ATN) itakuwa ikionesha matukio ya utalii kupitia skrini kubwa.

Aidha alitoa wito kwa mashirika binafsi kujitokeza katika kuwekeza kwenye miundombinu ya malazi kwenye maeneo yenye vivutio vya Utalii ili kuwavutia watu wanaotembelea.

Alisema kupitia kampeni hiyo mashindano mbali mbali yataendeshwa ambapo washindi watapelekwa kwenye hifadhi za Taifa kutembelea ikiwemo kujishindia zawadi mbalimbali.

UJUMBE KWA FACEBOOK