TTCL

Habari

TTCL YAJIPANGA KUTOA GAWIO SHILINGI BILIONI MOJA KWA HUDUMA ZA KIJAMII

on

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mbeya wakishiriki katika Tamasha la Shika Ndinga lililodhaminiwa na Shirika la Mawasiliano la TTCL

 

Meneja wa Shirika la Mawasiliano Mbeya na Songwe Florence Mtuka akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa Tamasha la Shika Ndinga Jijini Mbeya

Meneja Masoko wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Aron Msonga akielezea mikakati ya TTCL kuwahudumia wakazi wengi kwa wakati

Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Florence Mtuka akitoa zawadi kwa mmoja wa washiriki 10 wa shindano la Shika Ndinga katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya.

Na Mwandishi wa MbeyaYetu

Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Mkoa wa Mbeya na Songwe limepanga kutoa gawio la Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kusaidia huduma za kijamii nchini.

Akizungumza wakati wa Tamasha maalumu la Shika Ndinga lililofanyika Viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya Meneja wa TTCL Florence Mtuka amesema gawio hilo ni sehemu ya faida zitokanazo na matumizi ya simu za mkononi kwa watumiaji.

Amesema Shirika hilo limekuja na Kauli mbiu ya ‘RUDINI NYUMBANI KUMENOGA’ ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuboresha huduma za mawasiliano na kuwarejesha watumiaji ambao walianza kutumia mitandao mingine ya simu.

Amesema TTCL imeboresha miamala ya fedha zinazofahamika kama TTCL PESA,kulipia bili za maji na Luku ambazo ni huduma za vifurushi kwa gharama nafuu ikiwa ni pamoja na bando la Waandishi Pack kwa ajili ya wanafunzi na Boom Pack kwa ajili ya wanafunzi.

Amefafanua kuwa zipo huduma za data na simu za kupiga kwa mikoa mikubwa ya Dar es salaam, Tanga,Dodoma,Arusha Mwanza, Zanzibar, Mtwara,Iringa na Mbeya,Singida, Kagera, Shinyanga, Kigoma na Tabora.

‘’TTCL tumebeba jukumu la kufikia katika maeneo isiyofikika mitandao mingine na ile ya pembezoni ambako hakukuwa na mawasiliano yoyote kabla yake’’amesema.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa TTCL Aron Msonga amesema Shirika la Mawasiliano TTCL limejipanga ifikapo Juni zaidi ya asilimia 80 ya watumiaji wawe wamefikiwa na huduma za Mobile za 4G,3G na 2G.

Msonga amesema kuwa TTCL imejipanga vyema kukabiliana na kuwa hakuna changamoto ambazo wanaweza kukutana nazo za mitandao mingine kwa kuwa TTCL ndiye inasimamia huduma za mawasiliano kwa mitandao mingine nchini.

‘’Sisi ndio wamiliki wa huduma za mitandao ya simu nchini na ndio tuliokuwa tunawagawia watoa huduma wengine,ndio maana huduma zetu ni nafuu kuliko mitandao mingine’’amesema Msonga.

Awali katika tamasha hilo la Shika Ndinga ambalo limedhaminiwa na TTCL kwa kushirikiana na Redio EFM ya jijini Dar es salaam kulikuwa na shindano maalumu la Shika Ndinga ambapo watu wawili wa kike na kiume walijinyakulia Bodaboda.

UJUMBE KWA FACEBOOK