TTCL

Habari

UBALOZI WA MAREKANI NCHINI KUSHIRIKIANA NA TAJATI

on

Afisa Habari kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini, Benjamin Ellis akizungumza na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utaliina Uwekezaji Tanzania (TAJATI)  Katibu Mkuu wa TAJATI, Venance Matinya, akisoma taarifa ya utendaji kazi wa Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji kwa Viongozi wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania  Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka Mwakilili akifafanua jambo kwa Maafisa Habari wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini. Maafisa Habari kutoka Ubalozi wa Marekani wakiwa katika kikao cha pamojana Viongozi wa TAJATI katika ofisi za Chama hicho jijini Mbeya Afisa Habari kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Benjamin Ellis akipokea taarifa ya utendaji kazi ya TAJATI kutoka kwa Katibu mkuu Venance Matinya Mtaalam wa Habari kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania akielezealengo la kutembelea Ofisi za TAJATI katika ziara yao ya hivi karibuni. Katibu Mkuu wa TAJATI, Venance Matinya akimuonesha Afisa Habari kutoka Ubalozi wa Marekani baadhi ya Picha za matukio ambayo yamefanywa na TAJATI na kuwekwa kwenye kumbukumbu Mkurugenzi wa Habari na mahusiano wa TAJATI, Felix Mwakyembe akifafanua jambo mbele ya Afisa Habari na Mtalaam wa Habari kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania. Mtunza hazina wa TAJATI, Brandy Nelson akiwapa zawadi ya Tsirt Afisa habari na Mtalaam wa habari kutoka Ubalozi wa Marekani baada ya kumaliza ziara yao katikaofisi za TAJATI zilizopo jijini Mbeya. Baadhi ya Viongozi wa TAJATI wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa habari na Mtalaam wa Habari kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini.

 

AFISA Habari kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Benjamin Ellis ameahidi kuhakikisha anashirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania katika kusimamia na kutangaza miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani Kanda ya Nyanda za juu kusini.

 

Afisa huyo ambaye aliambatana na Mtalaam wa Habari kutoka Ubalozi huo, Japheti Sanga alitoa ahadi hiyo jana alipofanya ziara ya kutembelea Ofisi za TAJATI zilizopo jijini Mbeya kwa lengo la kujua shughuli zinazofanywa na Chama hicho na kujenga mahusiano kati ya kitengo cha Habari chini ya Ubalozi na Wanahabari wa Tajati.

 

Alisema amefarijika kufika katika ofisi za Tajati na kujionea shughuli mbalimbali ambazo Chama hicho imezifanya ambazo zimechangia kuchochea ukuaji wa uchumi katika sekta za Utalii na Uwekezaji nchini.

 

Alisema atazungumza na uongozi wa Ubalozi ili kuhakikisha Miradi ambayo imefadhiriwa na Serikali ya Marekani na inayotekelezwa katika Mikoa ya ukanda wa Nyanda za juu kusini.

 

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na Sekta za afya, Elimu, Kilimo na kupambana na Uwindaji haramu dhidi ya wanyapori hivyo kutokana na shughuli za TAJATI ni vema ikashiriki moja kwa moja katika kufuatilia utekelezaji wake.

 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Tajati katika taarifa yake kwa Wageni hao alisema changamoto inayokikabili Chama hicho ni ukosefu wa vitendea kazi vitakavyowezesha kurahisisha kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutembelea maeneo yenye fursa za Utalii na Uwekezaji.

 

Naye Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka Mwakilili alisema Mfumo wa utekelezaji wa majukumu ya TAJATI unatokana na kufanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja kwa kuenda kwenye eneo la tukio kama timu hivyo kinachohitajika ni uwezeshaji wa vitendea kazi.

 

Alisema katika kazi zilizofanyika kwa miaka miwili tangu kuanzishwa kwake zilikuwa za kujitolea kwa wanahabari wenyewe hata hivyo zimekuwa zikileta mafanikio   kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

 

Awali Mkurugenzi wa Habari na mahusiano wa TAJATI, Felix Mwakyembe alizitaja baadhi ya kazi zilizofanywa na TAJATI na kuleta mafanikio kuwa ni pamoja na kuandika habari kuhusu kuvamiwa kwa uwanja wa ndege wa zamani uliopo jijini Mbeya na kuandika kuhusu fursa za Uwekezaji na Utalii katika hifadhi ya wanyama Kitulo.

 

 

UJUMBE KWA FACEBOOK