TTCL

Makala

USIYOYAJUA KUHUSU MAPOROMOKO YA RUSUMO  (Rusumo water Falls) NGAR A -KAGERA.

on

MAPOROMOKO ya  Rusumo ni moja ya maporomoko yanayomvutia  mgeni yeyote anayefika katika eneo la maporomoko hayo yaliyopo katika eneo la Rusumo wilaya ya  Ngara mkoani Kagera.

Uwepo wa maporomoko hayo unatokana na mto Kagera au Ruvubu   uliopo katika mpaka wa Tanzania na Rwanda na ni moja ya eneo ambalo ni kivutio kikubwa kwa wageni mbalimbali wanaofika katika ene hilo lililopo nje kidogo ya mji wa  Ngara.
Maporomoko hayo huonekana kwa chini ukiwa juu ya daraja linalotengaisha  nchi ya Tanzania na Rwanda  na yamekuwa kivutio kikubwa kutokana na maji yake kuporomoka kwa kasi sana.

Ukiwa katika eneo hilo si rahisi sana kuona mpaka chini kutokana na  mvuke  wa maji wenye muonekano wa ukungu  unaotokana na kasi ya maji yanayoporomoka  kutoka mto Kagera upande wa Ngara.
Wageni wanaovuka mpaka huo wa Rusumo  ni kawaida kukuta wakishangaa maporomoko hayo ya aina yake ambayo ni kivutio kikubwa cha kitalii.
Mbali ya maporomoko hayo kuwa maonyesho ya kuvuti ya kitalii,Kwa mjibu wa watafiti ni kuwa maporomoko hayo  ambayo chanzo chake ni mto Kagera au Ruvubu yana uwezo wa kuzalisha megawati 90 za umeme. 
Tangu mwaka  2013 serikali za Tanzania, Burundi na Rwanda zitiliana saini mkataba wa maridhiano ya pamoja katika kusimamia mradi mpya na mkubwa wa kuzalisha umeme  kwenye maporomoko  hayo ya maji  katika Mto Kagera uliopo wilaya ya Ngara.
Mradi huo uliopo chini ya Uratibu wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki (EAC), umefadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) kwa kiasi cha dora Milioni 340, na nchi hizo wananchama zinatarajia kunufaika na  nishati hiyo ya umeme na kila nchi itapata mgao sawa wa nishati hiyo. 
Ikumbukwe kuwa kabla ya malidhiano hayo, mradi huo uliwahi kuwa katika mipango ya kuendeleza umeme katika   miaka ya 1980 hadi 1990, mipango hiyo iliingiliwa na kile kilichotajwa kuwa ni  matumizi ya maji ya Mto Nile hivyo kukosa ufadhili  na kisha baadae vita vya wenye kwa wenyewe katika nchi za Burundi na Rwanda  zikadhorojesha jitihada hizo. 
Imeandaliwa na  Ng’oko Innocent

UJUMBE KWA FACEBOOK