TTCL

Habari

WAHASIBU WAPONGEZA MFUMO MPYA WA EPICOR 10.2

on

Afisa usimamizi wa fedha kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mmaka Mwinjaka akitoa maelekezo kwa Wahasibu wanafundishwa mfumo mpya wa Epicor 10.2 Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Asha Msangi akitoa maelekezo kwa washiriki wa mafunzo ya Epicor 10.2 yanayowahusu Wahasibu na Watunza hazina wa Halmashauri Mhasibu kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Asha Msangi akitoa maelekezo kwa washiriki wa mafunzo ya Epicor 10.2 yanayowahusu Wahasibu na Watunza hazina wa Halmashauri Afisa usimamizi wa fedha kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mmaka Mwinjaka akitoa maelekezo kwa Wahasibu wanafundishwa mfumo mpya wa Epicor 10.2 Washiriki wakifuatilia kwa makini somo kutoka kwa wawezeshaji Washiriki wakijinyoosha kidogo baada ya kupewa somo

 

WAHASIBU na Watunza Hazina kutoka Halmashauri za Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Songwe wamepongeza mfumo mpya wa uhasibu wa Epicor 10.2 kuwa utawaongezea ufanisi katika kazi.

 

Wahasibu hao wanaoshiriki mafunzo ya siku nne katika ukumbi wa Hoteli ya Usungilo jijini Mbeya wamesema awali katika masuala ya fedha walikuwa wakitumia mifumo ya Epicor 9.05, 10.1 na 7 ambayo ilikuwa na changamoto nyingi.

 

Edwin Michael mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe alisema mifumo ya awali ilikuwa haiwezi kuingiliana na mifumo mingine ya fedha ambapo Bajeti na Mapato yalikuwa hayawezi kuwasiliana.

 

Naye Mhasibu wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Mede Mwanidako alisema mafunzo ya Epicor 10.2 yamekuwa msaada sana kwani yatawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi pamoja na kuondoa mkanganyiko wa uhamishaji wa fedha.

 

Kwa upande wake Mhasibu wa Halmashauri ya Jiji Bertha Mwashubira alisema kwanza mafunzo yamemuongezea uelewa juu ya mifumo ya fedha jambo litakalomuongezea ufanisi katika utendaji wa kazi.

 

Alisema mfumo huo mpya utasaidia katika utendaji kazi kwani utaweza kuondoa usumbufu kwa mhasibu kuandika andika mara kwa mara na matumizi ya vitabu vya risiti.

 

Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mpakani Kalinga alisema mfumo huo mpya utarahisisha na kuondoa uhamishaji wa taarifa za fedha kutoka mfumo mmoja kwenda mwingine.

 

Alisema mfumo mpya pia utasaidia kwenye udhibiti na uwazi utaongezeka katika shughuli zinazohusu fedha ambapo pia utapunguza mwingiliano wa majukumu ya Wahasibu na Watunza hazina kama ilivyokuwa awali.

UJUMBE KWA FACEBOOK