TTCL

Michezo

WAKAZI MBEYA WAHAMASISHWA KUJIFUNZA MZIKI MTAKATIFU

on

Moja ya vifaa vya mziki vitakavyotumika kujifunzia.

MKURUGENZI wa Uchungaji wa Jimbo Katoliki la Mbeya, Fr. Sirilo Mwalyoyo kupitia Kampuni ya LFCC Media anawaalika na kuwahamasisha  Wakazi wa Jiji la Mbeya kujitokeza kujifunza muziki Mtakatifu.

 

Kwamujibu wa Mkurugenzi huyo, Masomo ya mziki Mtakatifu yatatolewa kuanzia Februari Mwaka huu katika madarasa ya Shule ya Msingi RuandaNzovwe iliyopo CCM Jijini Mbeya.

 

Alisema fani zitakazotolewa ni pamoja na kupiga kinanda, kusoma na kufundisha mziki (NOTA), kupiga ngoma, Kwaya masta, kutunga na kuandika nyimbo pamoja na kujifunza kuimba (Vocal).

 

Alisema sifaza kujiunga na Chuo hicho ni kwa mtu yeyote mwenye akili timamu anayejua kusoma na kuandika pa oja na kuwa na uaminifu na Imani.

 

Aliongeza kuwa muda wa masomo ni makubaliano baina ya Mwalimu na Mwanafunzi pia itategemea na wepesi wa mwanafunzi katika kushika na kuelewa vizuri masomo yake.

 

Alisema fomu za kujiunga zitapatiakana Shule ya Msingi RuandaNzovwe, Parokia ya Mtakatifu Yakobo Uyole, Parokia ya Roho Mtakatifu Ruanda, Parokia ya Bikira Maria wa Fatima au Kanisa la Hija Mwanjelwa  na Kanisa kuu la Mtakatifu wa Antoni wa Padua mjini.

 

Alisema fomu za kujiunga zinapatikana kwenye vituo hivyo kwa shilingi 5000 kwa fomu moja kulingana na kozi anayotaka kusomea au kwa kuwasiliana na Mwalimu kupitia simu namba 0755 068195 au 0625760230.

 

UJUMBE KWA FACEBOOK