TTCL

Habari

Wanafunzi wa Kike Mzumbe Kampasi ya Mbeya Wajengewa Uwezo wa Kujitambua

on

Bi Mariam Mattao-Mkurugenzi wa Ushauri wa Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe-Morogoro

Bi Zitta Gervas Mnyanyi-Mshauri wa Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya

Safina Methusela-Mwanafunzi na Mjasiriamali Chuo Kikuu Mzumbe-MbeyaBeatrice Michael-Mwanafunzi na Mjasiriamali Chuo Kikuu Mzumbe-MorogoroOliva Mahenge-Mwanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe-Mbeya Baadhi ya Wanafunzi wa Kike wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya

Wanafunzi waliohudhuria semina wa ajili ya kujengewa uwezo wa kujitambua na kujithamini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na walimu wao mbele ya maktaba ya chuo hicho Jijini Mbeya

 

Wanafunzi wa Kike wanaosoma katika vyuo mbalimbali nchini wametakiwa kujiamini, kujithamini ili kujiongeza thamani na kuepuka mambo ambayo yanaweza kuwaingiza katika majanga ya kimaisha.

Ushauri huo kwa wanafunzi umetolewa na Mkurugenzi wa Ushauri wa wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Morogoro Mariam Mattao wakati wa semina fupi ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike takribani 180 wanaosoma Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya.

Bi Mariam amewataka wanafunzi hao kuwa mfano katika jamii ikiwa ni pamoja na kujiepusha katika makundi na mchanganyiko usio na tija katika maisha yao baada ya kumaliza elimu ya Chuo Kikuu.

Mkurugenzi huyo wa ushauri kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe ametoa ushuhuda wa maisha yake namna ambavyo amekumbana na changamoto za kimaisha baada ya kufiwa na mumewe na kuwa pamoja na changamoto alizokumbana nazo alijitahidi kujiamini na kujithamini na kukabiliana na hatimaye kufanikiwa katika maisha.

Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Morogoro Dkt Nsubili Isaga amesema kuwa amesema kuwa wanafunzi wa kike wanatakiwa kuchagua kujituma na kufanya jitihada katika kile walichokichagua kukifanya ili kupata mafanikio katika maisha yao baada ya masomo ya chuo kikuu.

Aidha wanafunzi ambao wamefanikiwa Safina Methusela,Beatrice Michael ambao mbali na kuwa ni wanafunzi wa chuo wamesema kuwa wanajishughulisha na ujasiriamali ambao umewasaidia kwa namna moja na nyingine katika kujiendeshea maisha yao katika mazingira yote ya chuo na hata wanapokuwa nyumbani wakati wa likizo.

Awali  Mkurugenzi wa Ustawi wa wanafunzi Mzumbe Bi Mariam Mattao amesema kuwa lengo la kuwa na semina aina hii kwa wanafunzi wa kike zinasaidia kuwazindua vijana wa kike ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo katika maisha yao wanapokuwa katika vyuo vikuu kutokana na majanga wanayokutana nayo kutokana na maumbile yao.

Amesema kuwa amefanya semina aina hii katika chuo Kikuu Morogoro na Chuo Kikuu Mbeya ambapo pia amebainisha kuwa lengo lake ikiwezekana kufanya semina aina hii kwa wanafunzi wa kike katika vyuo vyote vikuu nchini ili elimu ya aina hii ienee kwa wanafunzi wote.

UJUMBE KWA FACEBOOK