TTCL

Habari

WANANCHI MKOANI MBEYA WAZIDI KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA USAJILI LICHA YA MVUA KUNYESHA KATIKA MAENEO TOFAUTI

on

Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambulsho vya Taifa Ndugu Lodrick Hawonga, akiwapatia wananchi wa Kata ya Ilemi huduma ya Usajili kwa kuwajazia fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa.

Maafisa Usajili – NIDA wakiwafanyia usajili wananchi waliofika katika Vituo mbali mbali vya Usajili kata ya ilemi, usajili unaohusisha uchukuaji wa alama za Kibaiologia, Saini ya Kielektroniki, pamoja na Picha, nyuma yao ni foleni ya Wananchi wakisubiri kupatiwa huduma hiyo

Baadhi ya Wananchi wa Vijiji mbalimbali kata ya Ilemi wakikamilisha usajili wa awali kwa kujaza fomu za maombi kwa wale ambao hawakuwa wamekamilisha zoezi hilo, kushoto ni Mjumbe wa kata hiyo Ndugu Martini Mpwani akiwasaidia kujaza barua za Utambulisho kwa wale waliokosa Viambatisho.

Mtendaji wa kata ya Ilemi Ndugu Amiri Kassimu, akiwahakiki na kuwatambulisha Wananchi wake kwa kuwagongea Muhuri wa Serikali ya Mtaa ya Ilemi pamoja na kuwaandikia barua za utambulisho zitakazowawezesha kukamilisha hatua muhimu katika zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa ambalo linahusisha uchukuaji alama za Vidole,  Picha na  saini ya Kielktroniki

Wananchi wakiwa wamepanga foleni nje ya moja ya Kituo cha Usajili wakisuburi kupatiwa huduma hiyo licha ya Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya.

Mmoja wa Wananchi waliojitokeza kupatiwa huduma ya Usajili katika kituo cha Usajili cha Mwamfute kata ya Ilemi akichukuliwa alama za Vidole katika zoezi la Usajili lililohusisha uchukuaji wa alama za kibailogia, saini ya Kielektroniki pamoja na Picha.

 

Licha ya Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Mbeya, Wananchi katika Kata na vijiji mbalimbali mkoani humo, wameendelea kuhamasika kujitokeza kwa wingi kusajili kupata Vitambulisho vya Taifa.

Katika Kata ya Ilemi amkusanyiko wa wananchi umekuwa mkubwa; ikidhihirisha ni kwa namna gani wananchi wamekuwa na uelewa mpana wa umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa; hususani katika kipindi hiki ambacho zoezi kwa sasa linaendelea.

Afisa Usajili Wilaya ya Mbeya Bi. Alavuya Ntalima amesema katika Kata ya Ilemi zoezi limeanza Jumatano tarehe 3/01/2018 na linahusisha Kata za Iganzo, Isanga, Sisimba, Mabarini, Maendeleo pamoja na Forest.

Wakizungumzia zoezi la Usajili linaloendelea katika Kata zao Watendaji wa Serikali za vijiji wameahidi   kuendelea kushrikiana kwa karibu na Mamlaka kuhakikisha wananchi wote wanaoishi kwenye vijiji vyao na wenye sifa wana sajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa ndani ya muda uliopangwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi wamepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) hususani hili la kuwatambua wananchi na kuwapatia Vitambulisho vya Taifa ambavyo vitawapa fursa ya kufanya mambo mengi na kutambulika katika shughuli mbalimbali za kijamii.

UJUMBE KWA FACEBOOK